Pages

Sunday, July 15, 2012

MISS SINZA 2012 ILIVYOFANA

Miss Sinza 2012, Brigita Alfred (katikati) akipunga mkono kwa furaha wakati akiwa na washindi wenzake, mshindi wa pili Judith Sangu (kushoto) na watatu Esther Mussa, baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kampuni ya SPM-Sufiani Photo Magic na Mtandao wa Sufianimafoto.blogspot,com, Nasma Sufiani, akimvisha taji na kumkabidhi zawadi Maria John, baada ya kuibuka kidedea katika shindano la kumska Sufianimafoto Miss Talent, lililofanyika ndano ya shindano hilo la Miss Sinza katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza jijini Dar es Salaam.
Sufianimafoto Miss Talent, Maria John, akiwa na furaha baada ya kuvishwa taji hilo na kukabidhiwa zawadi yake.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wanakamati wakishuhudia shindano hilo.
Mshiriki, Nancy, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
Mshiriki,Naima mohamed, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
Mshiriki, Maria John, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Msanii wa Vichekesho, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Uongo Kweli, akishambulia jukwaa, wakati wa onyesho hilo na kuwapagawisha vilivyo, mashabiki wa fani ya urembo waliokuwapo ukumbini hapo.
Mshiriki, Mariam Miraji, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
Sehemu ya watu waliojitokeza kushuhudia shindano hilo.
Madj wa Sufianimafo, wakiwa katika mitambo ya Sufianimafoto, iliyokuwa ikitumika katika shindano hilo, wakiendesha shughuli nzima ukumbini hapo.
Pozi la Masawe Mtata, kabla hajapanda jukwaani, huku akiwa ameketi na wanadada ambao baada ya kushuka jukwaani walianza kumgombea, ''he kumbe tumekaa na Masawe hapa hatujui, hebu nipe namba yako'', wasilikika madada hao wakisema kila mmoja akiomba namba huku mwingine akisikika kumpiga mkwara Masawe, ''Ole wako umpe namba huyo mdada ntakupasua'' alsema mdada mmoja kati ya hawa walionyuma yake kana kwamba yeye alikuwa tayari amekwisha wini kupata namba.
Waimbaji wa Twanga Pepeta, wakishambulia jukwaa.
Wanenguani na waimbaji wa Twanga, wakishambulia jukwaa.
Mshiriki, Mariam, akipita jukwaani na vazi la usiku.
Mshiriki, Maria John, akipita jukwaani na vazi la usiku.
Mshiriki, Ester Mussa, akipita jukwaani na vazi la usiku.
Warembo hao wakicheza shoo ya pamoja ya ufunguzi.
Sehemu ya watu waliojitokeza kushuhudia shindano hilo.
Masawe Mtata, akikamua jukwaani kibao chake cha Uongo Kweli.
Miss Sinza 2011, (kushoto) akipozi na wenzake ukumbini hapo.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya Tano Bora, wakipozi kwa picha, kutoka (kulia) ni Brigita Alfred, Judith Sangu, Nahma Said, Ester Mussa na Mariam Miraji, baada ya kutangazwa kutinga hatua hiyo.
Mshiriki, Naima Mohamed, akicheza kushindania taji la Sufianimafoto Miss Talent, lakini bahati haikuwa ya kumwagwa na Maria John.
Sufianimafoto Miss Talent, akionyesha umahiri wake wakati akiharalisha kutwaa taji hilo kwa kucheza wimbo mpya wa Tunda Man.
Mwalimu wa waremabo hao, Mwajabu Juma, akipita jukwaani kusalimia wadau wa urembo.
Warembo wakicheza shoo ya pamoja ya ufunguzi.
Mshiriki, Naima Mohamed, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Mshiriki, Ester Mussa, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Mshiriki, Mariam, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
Miss Sinza 2012, Brigita Alfred, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.

***************************************
Brigita Alfred atwa taji la Redds Miss Sinza 2012
Na Mwandishi Wetu
MREMBO Brigita Alfred usiku wa kuamkia jana alitwaa taji la Redds Miss Sinza baada ya kuwashinda wenzake 13 katika kinyang’anyiro kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star Lounge).
Brigita alionekana tokea mwanzo kuwa ataibuka uwa mshindi kwani aliuteka umati wa mashabiki wa masula ya urembo katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kinywaji cha Redds, Dodoma Wine, Lady Pepeta, Flexi P, Jackz Cosmetics, Clouds FM, sufianimafoto.blogspot.com na Screen Masters.
Kwa ushindi huo,Brigita alipewa shs 500,000 na tiketi ya kuiwakilisha Sinza katika mashindano ya Redds Miss Kinondoni. Mshndi wa pili katika kinyang’anyro hicho alikuwa Judith Sangu aliyezawadiwa sh. 400,000 na mshindi wa nafasi ya mshind wa tatu ilikwenda kwa Esther Mussa na kupewa shs. 300,000.
Mariam Miraji alishinda nafasi ya nne nay a tano ilikwenda kwa Nahma Saidi. Warembo wote hao watano walipata tiketi ya kushindana katika mashindano ya Miss Kinondoni.
Warembo wengine waliobaki, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Eva Mushi, Vailet John, Christina Samwel, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi na Merina Mushi walipewa zawadi ya kifuta jasho cha shs 100,000 ila mmoja katika shindano hilo lilopambwa na bendi ya African Stars wana Twanga Pepeta.

Popular Posts