Pages

Friday, July 20, 2012

Zoezi la Watu Mbalimbali Kutambua Miili ya Ndugu, Jamaa na Marafiki Zao Waliofariki Dunia Kutokana na Ajali ya Kuzama Kwa Meli ya Mv Skagit

Baadhi ya Maiti zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya Skagit iliozama zikiwa katika Eneo la Maisara kwa ajili ya kutambuliwa na Nduguzao.
Maiti zikihifadhiwa katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar tayari kwa utambuzi wa ndugu na jamaaa.
Wananchi mbalimbali wakizitambua Maiti zao zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Jamaa wa mmoja wa marehemu wa ajali ya Boti akiwa na simazi ya kuondokewa na jamaa yake katika tukio la ajali hiyo, baada ya kuitambua maiti ya jamaa yake iliopelekwa katika viwanja vya maisara.
Baadhi ya Wananchi waliozitambua maiti zao katika Viwanja vya Maisara wakisaidiwa na Askari kutokana na Huzuni kubwa waliokuwanazo.kwa kuzama kwa Meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika Foleni ili kwenda kuzitambua Maiti zao katika Viwanja vya Maisara kutokana na kuzama kwa Meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Baadhi ya Wanandugu wakiwa katika foleni kusubiri kutambua miili ya Ndugu zao waliopata ajali ya kuzama kwa boti ya Kampuni ya SeaGull.jana katika bahari ya Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika Foleni ili kwenda kuzitambua Maiti zao katika Viwanja vya Maisara kutokana na kuzama kwa Meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Wananchi wakiwa katika viwanja vya mpira Mairasa kusubiri kutambua miili ya jamaa zao.
Baadhi ya Wageni kutoka Nchi mbalimbali wakiwa katika Viwanja vya Maisara ili kujuwa Ndugu zao na kuangalia taratibu zinazofanyika viwanjani hapo kutokana na Kuzama kwa meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Baadhi ya Maiti zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya Skagit ilizama zikiteremshwa katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar ili kutambuliwa na Jamaa zao.

Popular Posts