Pages

Saturday, June 30, 2012

MWAKA 1984 WABUNGE WAKIPANDA BASI KWENDA BUNGENI DODOMA

Kugombana na Madaktari ni Uchuro

Mgomo wa madaktari umeanza tena, siku chache zilizopita. Inasikitisha kuona kuwa tumefikia hali hiyo. Ukiniuliza nani namhesabu kama mwajibikaji mkuu aliyesababisha tatio hili, nitakuambia kuwa ni serikali ya CCM. Huo umekuwa msimamo wangu tangu pale ulipotokea mgomo wa mwanzo wa madaktari wiki kadha zilizopita. Nilieleza msimamo huo hapa.

Siku chache zilizopita, nilimsikiliza mwenyekiti wa madaktari wanaogoma, Dr.Stephen Ulimboka, akiongelea jinsi uhaba wa vitendea kazi ulivyo. Alitaja mfano wa kifaa cha "CT-scan" ambacho kimeharibika Muhimbili yapata miezi mingi iliyopita.

Kama nilivyosema katika makala yangu ya mwanzo, sera za serikali ya CCM zinasabisha upotevu mkubwa wa mali ya Tanzania, kama vile madini. Serikali yenyewe imekiri kuwa mikataba ya madini ya siku zilizopita ilikuwa ni ya hasara kwa Taifa. Lakini je, serikali imeshamwajibisha yeyote aliyehusika katika kusaini mikataba hiyo?

Je, ni kweli kuwa nchi hii haiwezi kununua hicho kifaa cha "CT-scan"? Kutokana na sera mbovu za CCM, makampuni kama Barrick yanafaidika sana na dhahabu yetu wakati sisi, ukifananisha na mapato wanayopata wao, sana sana tunaambulia mapato duni sawa na njugu kiganjani, na tunaambulia uharibifu wa mazingira na afya za watu wanaoishi maeneo ya migodini,

Kitu kimoja kinachokera katika mgogoro huu baina ya serikali na madaktari ni jinsi madai ya madaktari yanavyopotoshwa. Wako ambao wanaongea kama vile wanachodai madaktari ni posho na maslahi yao tu. Ukweli ni kuwa madaktari wana madai ya msingi ya kuwatetea wananchi. Kuna uchakachuaji wa makusudi unaofanywa kuhusu jambo hilo, ili ionekane kuwa madaktari hawajali maishai ya wananchi.

Ni kweli kuwa mgomo huu unaathiri maisha ya wa-Tanzania. Hili si jambo jema. Lakini serikali haina haki ya kuwashutumu madaktari kwa hoja hii ya kutojali maisha ya wa-Tanzania, wakati serikali hiii hiii inawakumbatia hao wanaoitwa wawekezaji ambao wengi wao wanahujumu maisha na afya za wa-Tanzania, achilia mbali kuharibu mazingira maeneo ya migodini. Serikali ingekuwa haifanyi hayo, ingekuwa na haki ya kuwaandama madaktari kwa hoja hii ya kuathiri maisha ya wa-Tanzania.

Katika mgogoro baina ya serikali na madaktari, kuna pia suala la serikali kutumia mwanya wa sheria na uamuzi wa mahakama. Serikali haifanyi haki inapokwepa kuwajibika kwa yale yanayodaiwa na madaktari, madai ambayo ni ya kweli, na yako katika uwezo wa serikali na nchi yetu hii ambayo ina utajiri mkubwa. Kama suala ni sheria na maamuzi ya mahakama, sote tunakubali kuwa sheria ichukue mkondo wake.

Lakini kinachokera ni kuwa serikali inatumia mwanya huu kufunika kile ambacho sisi wengine tunakiona ni uzembe na kutowajibika kwa serikali yenyewe. Madai ya madaktari ni ya msingi, na yako katika uwezo wa serikali hii. Kwa serikali kutowajibika hapo na kukimbilia mahakamani kuwabana madaktari kwa kipengele cha sheria tu, sio jambo la haki na haliiweki serikali katika sura nzuri, kwa mtazamo wangu.

Kama nilivyosema katika makala yangu ya mwanzo, kugombana na madaktari si jambo jema. Nilikumbushia usemi wa wahenga kuwa tusidharau wakunga na uzazi ungalipo. Napenda kuongezea kwa dhati kabisa kuwa kugombana na madaktari si dalili njema bali ni uchuro.

http://hapakwetu.blogspot.com/

MISS UNIVERSE TANZANIA 2012

Yesterday night we witnessed the crowning of Miss Universe Tanzania 2012... at the National Museum Auditorium...the show was on point!!
So....the gorgeous Winfrida Dominic (center) won the Miss Universe Tanzania 2012 title...while Bahati Chando(left) was First Runners Up, and Dorice Mollel (right) is Second Runners Up. All the girls have earned a chance to represent Tanzania in different countries through Miss Universe, Miss Earth and Miss Queen International.
PHOTOS: http://missiepopular.blogspot.com

MAONYESHO YA BIASHARA YAFANA MKOANI IRINGA

Wajasiriamali kutoka Iringa wakionyesha ujumbe wao wakati wakipita mbele ya Waziri Mkuu
Fatma Kange akitoa maelezo juu ya umuhimu wa bar codes katika bidhaa za Tanzania kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda
Baadhi ya bidhaa kutoka kwa msindikizaji wa vyakula Lusiga's wa mkoa wa Morogoro

Balozi wa Rwanda nchini akimsikiliza akimsikiliza mjasiriamali Kibibi Japhary akifananua jambo juu ya mafuta na unga wa Ubuyu katikati ni Flora Ibreck wa TPSF

Bidhaa za Soya kutoka Gemji Home Bakery Healthy Bread zikiwa zimehifadhiwa katika viwango vya juu kabisa.

Ras Mizizi wa kikundi cha Wa Asili Asili akitoa maelezo kwa Mh. Waziri Mkuu, ndugu Mizengo Pinda juu ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi,katikati ni mwenyekiti wa TPSF Mama Esther Mkwizu

Asali safi ya Nyuki kutoka Pemba

Mama Eonike Sauli Lema wa Designer Boutique Fashion akionyesha baadhi ya kazi zake za mkono.

Redds Miss Ubungo 2012, Irine Sizari


Redds Miss Ubungo 2012, Irine Sizari (katikati) akipunga mono baada ya kuvukwa taji hilo na kupata tiketi ya kushiriki Miss Kinondoni 2012. Kushoto ni Mshindi wa Pili, Mwantumu Mustafa na kulia ni Mshindi wa tatu, Antonia Nyaragwinda. Shindano hilo limefanyika Juni 29, 2012 kuamkia Juni 30.
Source : Full Sangwe

MISS REDDS IRINGA 2012 ILIVYOKUWA

Huyu ndie Naomi James ambaye ametawazwa usiku huu kuwa Miss Redd's mkoa wa Iringa na kuzawadiwa kitita cha shilingi 500,000
Mshindi wa taji la Miss REdd's 2012 mkoa wa Iringa Naomi James kati kati akiwa na mshindi wa pili Sarah Utiku na Catherine Mfupi ambaye ni mshindi wa tatu mara baada ya kutangazwa usiku huu ndani ya ukumbi wa Highlands mjini Iringa
Msaidizi wa chifu jaji msomi Saimon Belenge akiokoa jahazi lisizame baada ya wadau wapenzi na mashabiki wa onyesho hilo kuanza kumzomea chifu jaji Bw Tasha Jimi ambaye ni mratibu wa Miss Redd's mikoa ya kusini baada ya kuchemka kutaja namba ya mshindi wa pili katika onyesho hilo
Hawa ndio waliopenya nafasi ya tano bora kati ya washiriki 12 waliopanda jukwani wa kwanza kushoto ni Amisa Zuber, SArah Utiku, Naomi James ,Winfreda Felix na Catherine Mfupi
Wadau wa urembo leo wakiwa wamevalia nguo za heshima kiasi
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja na washindi na washiriki wa onyesho hilo
Mgeni rasimi Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki ( wa pili kushoto) akiwa na afisa michezo na utamaduni Manispaa ya Iringa Bw.Kadinde na mratibu wa onyesho hilo Bw Dosi
Hawa ndio majaji wa onyesho hilo katikati ni Tasha Jimbo aliyetaka kuvuruga onyesho dakika za mwisho
Msomi Saimon Belege (kulia) akicheka baada ya chifu jaji kushoto TashaJimy kuvuruga kazi yao
Madau Saimon Belege akiwa na mshindi wa taji la Miss Iringa mwaka jana na mshindi wa leo katika shindano ya Redd's Miss Iringa Naomi James


Huyu ndiye Tasha Jimy aliyezomewa kwa kushindwa kujua tofauti kati ya namba 4 na mbili hivyo kujikuta akizomewa ukumbini.

KLABU YA SIMBA KUSHIRIKI KOMBE LA URAFIKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KLABU ya Simba inapenda kutangaza kuwa itashiriki katika michuano ya Kombe la Tanzania (Urafiki) iliyopangwa kuanza visiwani Zanzibar Jumatatu ijayo.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange, maamuzi ya kushiriki katika mashindano hayo yamefikiwa baada ya majadiliano baina ya uongozi, benchi la ufundi na Kamati ya Ufundi ya Simba.

“Tumeamua kushiriki kwa sababu tumeona haitakuwa vema kufanya hivyo wakati watu wa Zanzibar wametupa heshima kubwa ya kutualika kwenye michuano hii. Kombe la Tanzania lina maana kubwa kwa sasa kutokana na hali halisi ya kisiasa na kijamii iliyopo visiwani humo kwa sasa,” alisema.

Makamu alisema zaidi ya kushiriki michuano hiyo, Simba pia itatumia fursa hiyo kuweka kambi maalumu kwa ajili ya kujiandaa na Kombe la Kagame lililopangwa kufanyika kuanzia Julai 14 mwaka huu.

Pia, alisema Simba itatumia ziara hiyo kupeleka kombe la Ligi Kuu ya Vodacom kwa wana Simba wa Zanzibar ambao walichangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa ubingwa Vodacom na pia.

“Tusisahau pia kwamba kabla ya kucheza mechi yetu ya mwisho dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga ambayo tulishinda kwa idadi ya mabao 5-0, Simba ilikwenda kuweka kambi Zanzibar,” alisema Kaburu.

Simba itaanza michuano hiyo siku ya Jumatatu ambapo itacheza na Mafunzo ya Zanzibar katika pambano lililopangwa kufanyika usiku. Awali mechi hiyo ilipangwa kuchezwa Jumatatu jioni lakini imesogezwa mbele hadi Jumatatu usiku.

Jumla ya timu nane zinashiriki katika michuano hiyo ambapo Waekundu wa Msimbazi wapo katika kundi A lenye timu za Simba, Azam, Mafunzo na timu ya soka ya taifa ya vijana ya Zanzibar wenye umri wa chini ya miaka 23 (Karume Boys).

Simba na Express kucheza Taifa

MABINGWA wa soka wa Tanzania, Simba SC, wanatarajiwa kucheza na mabingwa wa soka wa Uganda, Express FC, katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopangwa kuchezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, maandalizi yote kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika na kwamba kikosi cha Simba kitaundwa na wachezaji wapya na wa zamani.


SIMBA SPORTS CLUB

P.O.BOX 15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330 |MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | EMAIL simbasportsclub@yahoo.com|

WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA

RATIBA YA KOMBE LA KAGAME 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) wataanza kutetea ubingwa wao Julai 14 mwaka huu dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye ametangaza ratiba ya michuano hiyo leo (Juni 29 mwaka huu) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Timu 11 zitashiriki katika michuano hiyo itakayoanza Julai 14 hadi 28 mwaka huu ambapo kwa siku zitachezwa mechi mbili (saa 8 mchana na saa 10 jioni) huku Tanzania Bara ikiwakilishwa na Yanga, Simba na Azam. Mechi ya kwanza siku ya ufunguzi (saa 8 mchana) itakuwa kati ya APR ya Rwanda na Wau Salaam ya Sudan Kusini.

Kundi A lina timu za Simba, URA ya Uganda, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Ports ya Djibouti. Azam, Mafunzo ya Zanzibar na Tusker ya Kenya ziko kundi B.

Yanga inaunda kundi C lenye timu za APR ya Rwanda, Wau Salaam ya Sudan Kusini na Atletico ya Burundi.

Timu nane zitaingia robo fainali itakayochezwa Julai 23 na 24 mwaka huu. Kundi A na C kila moja litatoa timu tatu kwenda robo fainali wakati B litatoa timu mbili.

El Merreikh ya Sudan, Red Sea ya Eritrea, Coffee ya Ethiopia na Elman ya Somalia hazitashiriki katika mashindano ya mwaka huu ambayo yanafanyika Tanzania Bara kwa mwaka wa tatu mfululizo kutokana na sababu mbalimbali.

Coffee haitashiriki kwa vile ligi ya Ethiopia inaanza Julai 14 mwaka huu wakati El Merreikh wikiend ya Julai 13-15 mwaka huu itakuwa na mechi ya michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Bingwa wa michuano hiyo atapata dola 30,000, makamu bingwa dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000. Michuano hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) na Televisheni ya SuperSport.

KAGAME CUP 2012 FIXTURE

Sat. 14th July 1 APR vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm

2 YANGA vs ATLETICO Uwanja wa Taifa 4pm

Sun. 15th July 3 AZAM vs MAFUNZO Chamazi 4pm

Mon. 16th July 4 VITA CLUB vs PORTS Uwanja wa Taifa 2pm

5 SIMBA vs URA Uwanja wa Taifa 4pm

Tue. 17th July 6 ATLETICO vs APR Uwanja wa Taifa 2pm

7 WAU SALAAM vs YANGA Uwanja wa Taifa 4pm

Wed. 18th July 8 VITA CLUB vs URA Uwanja wa Taifa 2pm

9 PORTS vs SIMBA Uwanja wa Taifa 4pm

Thu. 19th July 10 ATLETICO vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm

11 MAFUNZO vs TUSKER Uwanja wa Taifa 4pm

Fri. 20th July 12 PORTS vs URA Uwanja wa Taifa 2pm

13 YANGA vs APR Uwanja wa Taifa 4pm

Sat. 21st July 14 AZAM vs TUSKER Uwanja wa Taifa 2pm

15 SIMBA vs VITA CLUB Uwanja wa Taifa 4pm

Sun. 22nd July REST DAY

QUARTER FINALS

Mon. 23rd July 16 B2 vs C2

17 A1 vs C3

Tue. 24th July 18 C1 vs A2

19 B1 vs A3

Wed. 25th July REST DAY

SEMI FINALS

Thu. 26th July 20 Winner 16 vs Winner 17

Thu. 26th July 21 Winner 18 vs Winner 19

Fri. 27th July REST DAY

FINALS AND 3rd PLACE PLAY OFFS

Sat. 28th July 22 Loser 20 vs Loser 21

23 Winner 20 vs Winner 21

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

WASANII WA FILAMU WATOA MSAADA HOSPITALI YA BOMBO , TANGA



Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Jacob Steven "JB" wakiwa kwenye picha ya pamoja na Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga.Wasanii hawa wametembelea Hospitali ya Bombo mapela leo asubuhi kwa ajili ya kukabidhi msaada wa Vyandarua katika hospitali hiyo,ikiwa ni sehemu ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria unaopoteza maisha ya watanzania wengi katika maeneo mbali mbali ya nchini.Msaada huo umekabidhiwwa hospitalini hapo kwa hishani ya kampuni ya Bia Tanzania Kupitia kinywaji Chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.Picha na Othman Michuzi
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa wamezunguka kitanda cha Mmoja wa Mama aliejifungua watoto Mapacha katika Wodi ya Wazazi wa Hospitali ya Bombo Jijini Tanga mapema leo asubuhi wakati walipofika kutoa Msaada wa Vyandarua kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Kinywaji chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.Picha na Othman Michuzi

Msanii wa Bongo Movie,Mayassa Mrisho akikabidhi Chandarua kwa Mama aliejifungua watoto mapacha kwenye hospitali ya Bombo,Tanga mapema leo asubuhi.Picha na Othman Michuzi.

WANANCHI WA KIJIJI CHA ISYONJE WAUVUA UONGOZI MADARAKANI

Hii ni barua ya kukiri ufujaji wa pesa.
*Mtunza hazina akiri kufuja fedha za kijiji.
*Mkutano wavurugika.
*Waunda kamati ya kusimia kijiji hicho.
*Diwani afunga mkutano.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga,Rungwe.
Wananchi wa Kijiji cha Isyonje,Kata ya Isongole,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wamemvua uongozi,mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Venance Daima na halmashauri ya kijiji kizima kwa tuhuma za ubadhilifu wa mali na kutosimamia ipasanyo rasilimali za kijiji ikiwemo mianzi ya asili na mashamba ya kijiji.

Tuhuma hizo zimetolewa katika mkutano maalumu wa kijiji hicho uliofanyika Juni 28 mwaka huu mbele ya Diwani wa kata hiyo mheshimiwa Laurence Nyasa Mfwango,ambapo baada ya kupitia taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa na Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwana Ambokile Kinjisi na kubaini kuwa jumla ya shilingi 1,118,000 kufunjwa na mhasibu wa kijiji Bwana Michael Mbilinyi.

Aidha mhasibu huyo alipotakiwa kuonyeshwa pesa hizo zilipo alishindwa hali iliyompelekea kukiri kosa hilo na kuahidi kuzilipa Juni 29 mwaka huu baada ya kujiwekea dhamana ya shamba la miti.

Hata hivyo wananchi hao waliutupia lawama uongozi wa kijiji kwa kutosimamia mali ikiwa ni pamoja na uuzaji holela wa mianzi na ukodishwaji wa mashamba bila ridhaa ya wananchio na kutoitisha mikutano ya hadhara ikiwa ni kinyume na kanuni za Serikali ya kijiji.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya tuhuma hizo wananchi walimtaka mwenyekiti huyo na halmashauri yake kujiuzuru,ambapo walikubaliana na kijiji hicho kusimamiwa na kamati ya mpito,chini ya Afisa mtendaji wa kijiji Bwana Kinjisi.

Kutokana na wananchi kuchoshwa na uongozi huo baadhi yao waliondoka mkutanoni kwa hasira na viongozi wa kijiji kuacha viti vyao na kumuacha Diwani,ambaye alilazimika kufunga mkutano.baada ya mwenyekiti aliyeufungua mkutano huo na wananchi wakaridhia Kamati ya watu 10 kusimamia shughuli za kimaendeleo hadi uongozi mwingine utakapochaguliwa kwa mujibu wa kanuni za kijiji.

Waislamu waaswa kushiriki Sensa ya Makazi na Watu mwaka 2012

Taasisi ya masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania imeunga mkono kauli iliyotolewa hivi karibuni na Sheikh mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Simba ya kuwataka waislamu na watanzania kote nchini kushiriki kikamilifu katika Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya mwenyekiti wa jopo la masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania Sheikh Hamis Mattaka amesema hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa baadhi ya makundi yanayowahamasisha waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kutoshirika zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Amesema wao kama jopo la wanazuoni hawaoni tatizo la zoezi hilo kutokana na umuhimu wake kwa taifa na kuongeza kuwa Sensa ya watu na makazi ipo kwa mujibu wa sheria za nchi na imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jopo hilo limeiomba serikali kuweka sheria itakayozuia utoaji wa takwimu zinazohusu dini za watanzania zinazotolewa na vyanzo mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kuwa kipengele hicho si sehemu ya sensa nchini.

“Tunajua kuwa serikali ilikua na nia njema kukiondoa kipengele cha dini katika Sensa hapana budi nia njema hiyo ya serikali ilindwe kwa kuweka sheria itakayozuia kutoa takwimu zinazohusu dini za watanzania” amesema Sheikh Mattaka.

Amefafanua kuwa Sensa ya awali ya mwaka 1957 kipengele cha dini kilihusishwa na baadaye kuondolewa katika Sensa zilizofuata kwenye madodoso ya kukusanyia takwimu za kaya.

“Sisi kama jopo kila siku tunasema ili twende salama kama wananchi wa nchi hii ni wajibu wetu kuheshimu na kufuata sheria kwa maana ya kutii sheria bila shuruti, kwa hiyo tunasema Sensa ya watu na makazi ni jambo la kisheria si jambo la mitaani, hatuwezi kulumbana na kujadili jambo ambalo liko wazi kisheria na limepitishwa na wabunge tuliowachagua sisi wenyewe”

Amefafanua kuwa zoezi la Sensa ya watu na makazi litaiwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa kuwa na takwimu sahihi za watu na makazi, hali ya kipato cha kaya, vizazi na vifo na pia kuiwezesha serikali kwapatia huduma bora wananchi wake.

Katika hatua nyingine jopo la masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania imewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya katiba.

Aidha jopo hilo limewataka watanzania wote kwa ujumla kuitumia fursa hiyo muhimu kutoa maoni ambayo yataiwezesha nchi kupata katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi.

“ Sisi kama jopo la wanazuoni wa kiislamu tunawataka waislamu na watanzania wote kwa ujumla kuitumia fursa hii muhimu kwa kutoa maoni yao ili hatimaye nchi yetu ipate katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi ijayo” amesema Sheikh Mattaka.

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA WATENDAJI WAKUU WA MAKAMPUNI MBALIMBALI YA KIMAREKANI WANAOTEMBELEA TANZANIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Kimarekani na waalimu wao pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe John Haule, Balozi wa Marekani nchini, Mhe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar. Wanafunzi hao wanachukua masomo ya lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zanzibar ( SUZA). Walikuwa wameongozana na Watendaji Wakuu wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania Marekani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour) iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania Marekani. Hii ni mara ya pili kufanyika ziara kama hii, ambapo pamoja na kuwakaribisha tena Rais Kikwete alisema amefurahishwa sana kwa wageni hao kuchagua kutembelea hifadhi za wanyama za kusini mwa nchi (Selous na Ruaha) vyenye wanyama wengi na vivutio ambavyo havipatikani kwingine kokote kama vile makundi ya mbwa mwitu ambayo kwa muda mrefu sasa yametoweka mbuga za Kaskazini.Picha na IKULU

UZINDUZI WA KINYWAJI CHA KIBO GOLD WAFANA

Kinywaji cha Kibo Gold kilichopotea kwa wanywaji wake takribani miaka kumi,kimerejeshwa tena kampuni ya bia ya Serengeti.
Meneja wa kinywaji cha bia ya Serengeti,Allan Chonjo akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa utambulisho mpya wa kinywaji cha Kibo Gold.Akizungumza na wageni waalikwa na waandishi wa habari waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika katika kiwanda cha Serengeti tawi la moshi mkoani Kilimanjaro, Bw.Allan Chonjo amesema kuwa kampuni yao imeamua kukizalisha kinywaji hicho na kukirejesha tena kwa wanywaji wake ambao walikikosa kwa muda wa miaka kumi tangu kilipoachwa kuzalishwa.
Meneja wa Kampuni ya Sbl,tawi la Moshi,Bw.Gerald Mandala akitoa historia fupi kuhusiana na na kinywaji cha Kibo Gold,kwa wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wanahabari (hawapo pichani),wakati wa utambulisho mpya wa kinywaji hicho uliofanyika kwenye viunga vya kiwanda hicho cha SBL Moshi.kuliwa kwake ni Operesheni Meneja wa Kiwanda,Bi.Alice Kilembe.
Mpishi wa bia ya Kibo Gold,Bw.Julius Nyaki akifafanua jambo kuhusiana na upishi wa kinywaji cha Kibo Gold bia.
Baadhi ya Wafanayakazi wa kampuni ya bia ya SBL wakishangweka vilivyo jioni ya leo na kinywaji chao kipya aina ya Kibo Gold,mara baada ya kukizindua tena kwa wakazi wa mji wa Moshi na kwingineko,mara baada ya kupotea kabisa kabisa katiko soko kwa muda wa miaka kumi.
Sehemu ya wageni waalikwa wa wakiwemo Wanhabari wakishuhudia utambulisho mpya wa kinywaji cha Kigo Gold uliofanyika leo jioni kwenye viunga vya kiwanda hicho,mjini Moshi.
Meneja wa bia ya Serengeti,Bwa.Allan Chonjo akimsikiliza mmoja wa wanyaji wa bia ya Kibo Gold kwa miaka miaka,akitoa ushuhuda wa urejesho mpya wa kinywaji hicho kwa wanywaji wake,ambapo anakiri wazi kuwa waliokuwa wanywaji wa bia hiyo wamefarijika sana kurejeshewa kinywaji chao walichokikosa kwa miaka mingi,takribani miaka kumi mpaka sasa.
Baadhi ya wafanyakazi wa SBL wakifurahi jambo kwa pamoja.
Wafanyakazi,wadau mbalimbali wakiwemo na wahahabari wakiw kwenye moja ya ukumbi wa kampuni ya SBL,mjini Moshi jioni ya leo kushuhudia utambulisho mpya wa kinyaji cha Kibo Gold.
Baadhi ya wadau wa kampuni ya Bia ya SBL,wakiwa kwenye utambulishao mpya wa kinywaji cha Kibo Gold,uliofanyika jioni ya leo kwanye viunga vya kampuni hiyo,mjini Moshi.

Friday, June 29, 2012

HALI YA DR STEVEN ULIMBOKA INAVYOZIDI KUIMARIKA

Hali ya afya ya Dkt. Steven Ulimboka inaendelea vyema baada ya kushambuliwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.Ulimboka anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhumbili (MNH), Kitengo cha mMifupa (MOI) aliko lazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku jopo la madaktari Bingwa wakiendelea kumnusuru Kama aonekanavyo pichani juu.Picha na Mdau Dande Francis

JUU YA USAJILI WA MELI ZA NJE ULIOFANYWA NA SMZ

TAARIFA KWA BARAZA LA WAWAKILISHI JUU YA
USAJILI WA MELI ZA NJE ULIOFANYWA NA SMZ
KUPITIA MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI
ZANZIBAR MARITIME AUTHORITY – ZMA
Friday, June 29, 2012

Mhe. Spika,
Tarehe 27/06/2012 Vyombo vya Habari hapa Tanzania (The Citizen) na nchi za nje (International news Agency – Bloomberg) viliandika makala kuhusu usajili wa meli 10 za mafuta (Tankers). Ilidaiwa katika makala hayo kuwa Meli hizo zilisajiliwa Zanzibar na zinapeperusha Bendera ya Tanzania na kwamba zinafanya biashara na Kampuni ya Serikali ya IRAN. Gazeti la “The Citizen la tarehe 27 Juni, 2012 lilikuwa na kichwa cha habari “Iran Tankers adopt TZ Flag to avoid embargo” (meli za mafuta za Iran zinatumia bendera ya Tz kukwepa vikwazo.

TAARIFA YA ZMA

Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar Maritime Authority – ZMA ni Mamlaka iliyoundwa kwa sheria No. 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na kazi nyengine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari Zanzibar ya mwaka 2006 (Zanzibar Maritime Transport Act 2006).

Sheria ya Zanzibar Maritime Transport Act 2006, kifungu no. 8 cha sheria hii, kinasomeka kama ifuatavyo:

Section 8 (1). There shall be established the registers of Tanzania Zanzibar ships to be Known as:-

o (a). Tanzania Zanzibar International Register of Shipping for ocean going ships; and

o (b) Tanzania Zanzibar Register of Shipping for coastal Ships.

• (2). A ship shall be a Tanzania Zanzibar ship for the purpose of this Act if that ship is registered under this part.

Katika kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama ilivyoelekezwa katika kifungu 8(1)(a) hapo juu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa. (Open Registry). Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa ZMA kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, General cargo na meli za Abiria.

Kama nilivyoeleza hapo awali, vyombo vya habari vimechapisha makala ya usajili wa meli 10 ambazo zinadaiwa ni meli za IRAN kulingana na makala zao hizo.

SMZ inatoa taarifa rasmi juu ya meli za mafuta ilizosajiliwa wiki mbili zilizopita pamoja na majina ya meli, ukubwa wake, majina ya makampuni inayomiliki meli hizo na nchi zilizotoka kabla ya kupata usajili kwa ZMA, kama ifuatavyo:

Jina la meli GRT (Ukubwa) Company name Ilikotoka

1. Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd Malta

2. Justice 164241 Justice Shipping Co. Ltd Cyprus

3. Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd Malta

4. Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd Malta

5. Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd Cyprus

6. Companion 164241 Companion Shipping Co. Ltd Malta

7. Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd Malta

8. Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd Malta

9. Courage 163660 Courage Shipping Co. ltd Cyprus

10. Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd Cyprus

11. valor 160930 valor Shipping Co. Ltd. Cyprus

Jumla ya GRT ni 1,388,368 tons

Meli hizi ni 11 kama zinavyoonekana katika orodha hapo juu ni miongoni mwa meli nyingi zinazobadilisha usajili wao (De registration). Meli zilizosajiliwa na ZMA zinatoka nchini Cyprus na Malta. Sambamaba na meli hizi 11 zilizosajiliwa na ZMA, meli za mafuta nyengine 20 ambazo zinasemekana zilikuwa kwenye usajili wa nchi za Ulaya zimebadilisha usajili wao na kwenda usajili wa “TUVALU Islands”.

ZMA ilimtaka Wakala wake Philtex Corporation kuwaita wenye meli hizi na kuwataka kujieleza kuhusu uhusuiano wao na Serikali ya au makampuni ya mafuta ya IRAN. Philtex ilikutana na Wamiliki hao siku ya Alkhamis tarehe 28/06/2012 katika afisi za Philtex Corporation na Wamiliki hao wameeleza kwamba hawana uhusianao na Serikali au mamlaka yoyote nchini Iran na wameamua kuja kusajili meli ZMA kwa ridhaa yao na kwa kufata matangazo ya usajili wetu wa nje (Open Registry).

Pamoja na maelezo hayo, wamiliki hao wametangaza kwamba ikiwa ZMA haiko tayari kuendelea na usajili wa meli zao, wanaweza kufuta usajili wao na tayari wanafikiria kufanya mazungumzo na open Registry nyengine (PANAMA) lakini hawana nia ya kurudi walikotoka, yaani Cyprus na Malta.

Kinyume na maelezo yaliyotolewa na vyombo vya habari juu ya uraia wa wamiliki wa meli hizi, Wamiliki wa meli hizi kama walivyojieleza katika usajili wa meli zao wana uraia wa British Vergin Islands na Sychelles.

Kulingana na “United Nations Convention Law of the Sea”, Article 91, na za “Geneva convection of Registration” articles 6, 7 na 8, na kulingana na Zanzibar Maritime Transport Act of 2006, section 8, Zanzibar ikiwa ni nchi moja kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo haki ya kusajili meli yeyote kulingana na taratibu na Sheria za Zanzibar, na sheria za Kimataifa zinazoongoza usajili huo.

Maelezo haya yanatolewa ili kutoa usahihi wa uvumi kuwa Zanzibar imesajili meli za IRAN ambazo zimewekewa vikwazo na Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya (European Union) juu ya usafirishaji na uuzaji wa mafuta kutoka Iran.

Mhe. Spika, taarifa hizi za vyombo vya habari hazina madhumuni yeyote zaidi ya kuwavunja moyo wenye Makampuni ya meli wanaotaka kusajili meli zao kwetu.

Hivyo basi Serikali inatamka wazi kwamba Usajili uliofanywa kwa meli hizi umefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria na kwamba Serikali imekuwa ikifanya na itaendelea kufanya mazungumzo na wenye meli mbalimbali ili kuongeza idadi na ukubwa wa meli inazosajili nje ya nchi. Biashara hii ya ukubwa wa GRT 1,388,368 Tons katika kipindi cha wiki mbili na maombi mapya matano kwa meli zitakazokuwa na ukubwa wa zaidi ya GRT 500,000 imeshtua Makamuni mengine na hata nchi nyengine zisizoitakia mema Zanzibar katika juhudi zake za kukuza mapato na uchumi wake.

Hata hivyo mamlaka itafata sheria zote zilizowekwa kitaifa na kimataifa katika biashara ya usafiri baharini na itahakikisha meli zinasajiliwa chini ya mamlaka hii zinafata taratibu ilizoweka.

Mhe. Spika, kabla ya taarifa hizi za vyombo vya habari (The Citizen), Waziri wa Uchukuzi wa SMT Mhe. Harisson Mwakyembe) alipokuwa akijibu suala Bungeni hivi juzi hakuonyesha kurishika kwake katika usajili wa meli (Open Registry) inayofanywa na Zanzibar na kuahidi kufanya ziara ya kuja Zanzibar kuonana na Waziri anaehusika kuzungumzia suala hili. Taarifa za “The Citizen” zaweza kuwa ni muendelezo wa Mhe. Mwakyembe kutoridhika kwake katika usajili unaofanywa na Serikali kupitia uwakala wake huko Dubai.

Mhe. Spika, Zanzibar haifungiki kusajili meli za nchi yeyote.

Hili ni suala la kibiashara na kwamba kwa Serikali yetu ni njia moja ya kuongeza mapato yanayoendesha Serikali, alimradi tu usajili huo hauvunji sheria za Kimataifa.

Mhe. Spika,

Zanzibar ina uhusiano mkubwa na wa muda mrefu na nchi nyingi ikiwemo IRAN na hivi karibuni Zanzibar ilipata ugeni (Makamo wa Rais wa Iran) na viongozi wetu walifanya mazungumzo ya namna gani IRAN itaendelea kusaidia Zanzibar katika miradi ya Maendeleo. Zanzibar haingependa kuingizwa kwa visingizio vyovyote na kwa njama zozote katika migogoro isiyowahusu.

Hivyo, kwa taarifa hii, Serikali inakanusha rasmi uvumi wa vyombo vya habari kuhusiana na suala hili kama taarifa hii ilivyofafanua hapo juu.

Mhe. Spika, naomba kuwasilisha.

Hamad Masoud Hamad

WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO

Chanzo: Zanzinews

U.S. Ambassador to Tanzania Ambassador Alfonso E. Lenhardt Celebrates 236th Anniversary of American Independence,Honors Tanzanian Youth

U.S. Ambassador to Tanzania, Alfonso E. Lenhardt,) (left), welcomes Chairman, Zanzibar House of Representatives Mzee Ali Mzee, (right), Former during the 4th of July celebrations held recently at the Chief of Mission Residence.
U.S. Ambassador to Tanzania, Alfonso E. Lenhardt, (left), welcomes the IPP Media Executive Chairman, Mr. Reginald A. Mengi, (right), during the 4th of July celebrations held recently at the Chief of Mission Residence.
U.S. Ambassador to Tanzania, Alfonso E. Lenhardt, (forth from left), pose for a photo with the Permanent Secretary form the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Mr. John Haule, (forth from right), and the winners of essays and paintings after having a toast during the 4th of July celebrations held recently at the Chief of Mission Residence.
---
In celebration of the 236th anniversary of American Independence, United States Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt hosted a reception at his residence on June 27 in Dar es Salaam.

The theme for this year's celebration centered around youth leaders as the future of Tanzania. The youth were represented by primary and middle school student winners of an essay contest - around the theme of "what democracy means to me," and an art contest - with the theme of "the leader I most admire." The evening also included performances by a U.S. Navy Band, the Kijitonyama Lutheran Youth Choir, and concluded with a spectacular fireworks display.

Before an audience of approximately 1000 Tanzanian government, business and cultural leaders, members of the diplomatic corps and other guests, Ambassador Lenhardt noted: "As President Barack Obama and Secretary of State Hillary Rodham Clinton have stated, youth outreach is one of the United States' top foreign policy priorities. This is because regardless of their social or economic background, it is the youth who will assume leadership roles in all sectors and shape the future of their nations, including in Tanzania. My message to them is that they can count on the United States as a strong partner and friend to strengthen Tanzania's democracy and ensure a future of progress and prosperity for all citizens."


"The United States-Tanzania partnership is based on mutual respect and mutual responsibility. In my many trips throughout this great country, I have met Tanzanians committed to building up their nation. Young leaders and Tanzanian patriots who partner with youth from Zanzibar and the mainland to mentor and empower them to promote development, entrepreneurship, and women's rights in their communities… These leaders and others like them know that the future of Tanzania is up to Tanzanians, not foreign donors. This spirit of self-reliance and national pride are among those values our two countries share," Ambassador Lenhardt said.


The Government of Tanzania was represented at the Fourth of July celebration by Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs John Michael Haule, who underscored in his speech the long-term ties of friendship and cooperation between both nations.

Tanzanian youth were represented by contest winners from the English Access Micro-scholarship Program students Lisa Geophrey, John D. Tinuga, and Ninah Mangesho for the essay contest. The Access Program's length is two years and aims to improve English language skills in talented students between the ages of 14 through 18.

The art contest winners included Makongo Primary School students Pascal Timothy, Daniel Charles, and Laurent Haji - all of whom selected Mwalimu Julius K. Nyerere as the leader they admired most and painted pictures of him.

The art work was displayed and the essays were available for guests to read on Kindle eReaders throughout the reception. Ambassador Lenhardt presented cash prizes and certificates to the essay and art contest winners at a ceremony held at the U.S. Embassy on June 25.

Dkt, Asha-Rose Migiro Ateuliwa Kuwa Mjumbe Wake Maalum katika Masuala ya Ukimwi na Ugonjwa wa Ukimwi Barani Afrika.

Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati wa hafla hiyo, akatoa shukrani zake kwa Ban ki Moon kwa kumpatia heshima hiyo ya kihistoria ambayo haita kaa ifutike na kwamba ameupokea uteuzi huo kwa mikoni miwili na hasa kutokana na kwamba tatizo la ugonjwa wa ukimwi ni tatizo ambalo analichukulia kwa uzito wa aina yake.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake Dkt. Asha-Rose Migiroakiteta jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akkisoma hotuba yake wakati wa hafla ya muaga naibu katibu mkuu aliyemaliza muda wake Dkt, Asha-Rose Migiro wa kwanza Kulia
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake, Dkt, Asha-Rose Migiro akimpiga picha Mwanae Pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon
--
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amemteua Naibu Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Dkt, Asha-Rose Migiro kuwa mjumbe wake maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi Barani Afrika.
Ban Ki Moon ametangaza uteuzi huo wakati wa hafla maalum aliyoiandaa mahsusi kwaajili ya kumuaga Naibu Katibu Mkuu wake,ambaye anahitimisha utumishi wake wa miaka mitano na nusu katika nafasi ya Unaibu katibu Mkuu.
Hafla hiyo imefanyika siku ya alhamisi katika viunga vya Umoja wa Mataifa, na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali wakiwamo mabalozi na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
“Ninatangaza rasmi kwamba ninamteua dkt. Asha- Rose Migiro kuwa mjumbe wangu maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa Ukimwi Barani Afrika. Akasema Ban Ki Moon tangazo lililoshangiliwa kwa nguvu na wageni waalikwa.
Akiongea kwa hisia, Ban Ki Moon, ameeleza kwamba ingawa Migiro alikuwa naibu katibu mkuu wake, lakini amekuwa mwalimu wake, amejifunza mengi toka kwake na daima ataendelea kuenzi mchango wake mkubwa.
“ Kama ni kuvaa viatu vyake, naweza kusema ningechekesha sana, kwa ufupi siwezi kuvaa viatu vya Migiro, amekuwa msaada mkubwa sana kwangu, ameniwakilisha vema kila mahali nilipomtuma hata katika mazingira magumu na ya hatari, kote ameniwakilisha vema sana, kama mwalimu wangu, na kama profesa wangu anastahili alama ya juu sana” akasema Ban Ki Moon na kushangiliwa.

Akamuelezea Migiro kama kiongozi si tu mwadilifu, lakini mwanadiplomasia aliyebobea, aliyefanya kazi kubwa,ngumu na nzito kwa moyo mkunjufu, uhodari , umakini, na uadilifu wa hali ya juu sana.
“ Siyo rahisi kuelezea yale aliyoyafanya nyuma ya pazia, namna gani alivyochapa kazi kwa nguvu, yapo mengi makubwa ambayo Migiro ameyafanya na kuyakamilisha kwa uadilifu wa hali ya juu.
Migiro ni mwanadiplomasia aliyebobea lakini ni mtu wa vitendo, vitendo ambavyo lazima utaona matunda yake” akabainisha Ban Ki Moon na kuongeza “ Migiro amefanya kazi na viongozi wagumu, kiwamo aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Quadaff aliyethubutu hata kumrushia katiba ya Umoja wa Mataifa, amezikuna nyonyo za watu wengi wakiwamo watu wanyonge na wenye matatizo mbalimbali. Migoro unaondoka, lakini Umoja wa Mataifa hauta sahau mchango wako. Hapa ni nyumbani kwako, na nitaendelea kuomba msaada wako na ushirikiano wako, bado nitaendelea kukuhitaji” akasisitiza Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akatumia fursa hiyo kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kumruhusu Migiro kwenda kuitumikia jumuia ya kimataifa.
“ Ninapenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa kumtoa Migiro katika utumishi wake wa Umma kuja kunisaidia , kwa serikali ya Tanzania na watanzania nasema asanteni sana” akasema Ban Ki Moon..
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu dkt. Asha-Rose Migiro amesema anaupokea kwa mikono miwili uteuzi wa kuwa mjumbe maalum wa Katibu Mkuu katika masuala ya Ukimwi.
Akasema masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi, ni eneo ambalo limo ndani ya moyo wake na kwamba anashukuru kuona kwamba Katibu Mkuu anamuamini kwamba anaweza kumsaidia. Akaahidi kwam atalitekeleza jukumu hilo kwa heshima kubwa.
Akamshukuru Ban Ki Moon, kwa kumuamini kwamba anaweza kumsaidia kama naibu Katibu Mkuu, na akamshukuru pia kwa ushirikiano mkubwa na uhusiano mkubwa uliojengeka kati yake na Ban Ki Moon lakini pia kati yake na wasaidizi wake. Ushirikiano ambao anasema ulichagiza utendaji kazi kufanikisha dira na matarajio ya Katibu Mkuu.
“Katibu Mkuu amenipa heshima ya kihistoria, heshima ya kuwa msadizi wake, ni heshima kubwa kwangu na kwa yeyote atakayekuja kuandika historia yangu, kwa namna yoyote ile hawezi kukwepa kumtaja Ban Ki Moon, naomba nikushukuru sana kwa heshima hii kubwa uliyonipa” akasema Migiro.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na familia ya Naibu Katibu Mkuu ikijumuisha mume wake, Profesa Cleophas Migiro, mdogo wa Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina Mtengeti na mtoto wa mwisho wa Migiro Chansa Jasmin.
Naibu Katibu Migiro anakuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo na mwanamke mwafrika wa kwanza. Lakini pia ni naibu katibu mkuu ambaye amehudumu katika wadhifa huo kwa miaka mitano na nusu.

Popular Posts