Pages

Saturday, September 1, 2012

Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete mwisho wa mwezi Agosti 2012

HOTUBAYA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 AGOSTI, 2012

Utangulizi
NduguWananchi;
Kilamwisho wa mwezi nimekuwa nazungumza na taifa kuhusu masuala mbalimbali muhimukwa taifa letu na watu wake. Leo ninamambo mawili ya kuzungumza nanyi. Lakini, kama ilivyo mazoea yetu hatuna budi kwanza tumshukuru MwenyeziMungu, muumba wetu, kwa kutujaalia baraka zake, za uhai na uzima na kutuwezeshakuwasiliana leo tarehe 31 Agosti, 2012.

NduguWananchi;
Jambola kwanza ninalotaka kuzungumzia leo ni zoezi la Sensa ya Watu na Makazilililoanza tarehe 26 Agosti, 2012 ambalo linatarajiwa kumalizika tarehe 01Septemba, 2012. Mtakumbuka kuwa tarehe25 Agosti, 2012 nilizungumza nanyi na kuwaomba mjitokeze kwa wingi na muwapeushirikiano unaostahili Makarani wa Sensa watakapopita majumbani mwenukutekekeza wajibu wao. Tumebakisha sikumoja kufikia kilele cha sehemu ya kwanza ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka2012.

Napendakuwashukuru kwa dhati Watanzania wenzangu wote kwa kujitokeza kwa wingikuhesabiwa. Mpaka sasa mwelekeo ni mzurina ugumu ulioonekana kuwepo pale mwanzoni uliendelea kupungua siku hadi sikukadri utekelezaji wa zoezi ulivyokuwa unaendelea. Kwa mwenendo huu nina matumaini makubwa kuwaSensa ya mwaka huu itakuwa na mafanikio mazuri.

Ndugu Wananchi;
Napendakutumia nafasi hii kutoa wito kwa wale wote ambao hawajahesabiwa wafanye hivyo.Naomba waitumie siku moja iliyosalia yaani tarehe 1 Septemba, 2012 kufanyahivyo. Aidha, namuomba Mkurugenzi Mkuuwa Ofisi Kuu ya Takwimu ya Serikali ya Muungano na Mtakwimu Mkuu wa Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar kuhakikisha kuwa kasoro zo zote zilizopo mahali po potezinatafutiwa ufumbuzi ili mambo yakamilike bila upungufu wowote.

NduguWananchi;
Baadaya kazi ya Makarani wa Sensa kuhesabu watu kufikia kilele chake, tarehe 2Septemba, 2012, linaanza zoezi la kuwashughulikia wale ndugu zetu ambaowatakuwa bado hawajahesabiwa. Itakuwepofursa ya siku saba kwa watu hao kuhesabiwa. Watatakiwa wao wenyewe kupeleka taarifa zao kwa Wenyeviti wao waSerikali za Mitaa au Vijiji. Taarifahizo zitafikishwa kwa Kamishna wa Sensa kwa ajili ya kujumuishwa. Baada ya muda huo kwisha, zoezi la kuhesabuwatu litakuwa limefika mwisho. Yuleambaye atakuwa hakutumia fursa hizo mbili atakuwa amekosa kuingizwa katikahesabu ya Watanzania ya mwaka 2012. Napenda kuwasihi ndugu zangu, Watanzania wenzangu kutumia siku ya tarehe1 Septemba, 2012 kuhesabiwa na kamahapana budi basi tumia fursa ya kupeleka taarifa zako kwa Mwenyekiti wako waMtaa au Kijiji katika siku saba zinazofuatia siku hiyo ili nawe ujumuishwe.

NduguWananchi;
Baadaya kazi ya kuhesabu watu kwa namna zote mbili kufikia mwisho, itaanza kazi yauchambuzi na kuunganisha takwimu na taarifa zilizokusanywa. Kazi hiyo ni muhimu na ni kubwa hivyo inahitajiumakini na uangalifu wa hali ya juu sana, kwani ikikosewa zoezi zima la Sensalitaingia dosari. Nafarijikakuhakikishiwa na Viongozi wa Sensa na Wakuu wa Idara za Takwimu za Serikalizetu mbili, kwamba wanatambua ukweli huo na wajibu wao. Wameniarifu kwamba kama mambo yatakwenda kamailivyopangwa, matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi kuhusu idadi ya watuna jinsia zao yatatolewa mwishoni mwa mwaka huu. Taarifa nyingine zitafuatabaadaye. Narejea kuwasihi Watanzaniawenzangu kuwapa nafasi wataalamu wetu wafanye kazi yao kwa ufanisi ili tupatematokeo yaliyo sahihi.
Mpakana Malawi
NduguWananchi;
Jambola pili ninalotaka kuzungumza nanyi leo ni kuhusu mpaka baina ya Tanzania naMalawi katika Ziwa Nyasa. Kama mjuavyo, kwamiaka mingi nchi zetu mbili zinatofautiana kuhusu wapi hasa mpaka uwe. Sisi, Tanzania, tunasema mpaka upo katikatiya ziwa wakati wenzetu wa Malawi wanasema upo kwenye ufukwe wa ziwa upande waTanzania. Kwa maneno mengine wanasema ziwalote ni mali ya nchi yao.

Utata kuhusu mpaka wetu katika ZiwaNyasa haujaanza leo. Ulikuwepo tanguwakati nchi zetu mbili zikiwa bado zinatawaliwa na wakoloni na kuendelea baadaya Uhuru wa nchi zetu mpaka sasa. Jambokubwa lililo tofauti na jipya ni kwamba hivi sasa, nchi zetu mbili zimeamuakukaa mezani na tunalizungumza suala hilo.
Chimbukola Mzozo
NduguWananchi;
Chimbuko la mzozo wa mpaka ulioposasa, baina ya nchi zetu mbili jirani, rafiki na ambazo watu wake ni ndugu, nimakubaliano baina ya Waingereza na Wajerumani kuhusu mpaka baina ya nchi zetuyaliyofanywa tarehe 1 Julai, 1890. Makubalianohayo yajulikanayo kama Mkataba wa Heligoland, (The Anglo-Germany HeligolandTreaty) yalitiwa saini kule Berlin, nchini Ujerumani baina ya Waingereza naWajerumani. Wakoloni hao walikubalianakuhusu mipaka baina ya makoloni yao na baina yao na wakoloni wenginewaliopakana nao. Kwetu sisi hayo ndiyomakubaliano yaliyoweka mipaka ya Tanganyika na ile ya Zanzibar na majirani zake. Kwa upande wa Ziwa Nyasa, Waingereza naWajerumani walikubaliana kuwa mpaka uwe kwenye ufukwe wa nchi yetu. Kwa maana hiyo ziwa lote likapewa nchi yaMalawi. Kwa upande wa Mto Songwe mpakaulikuwa ufukweni upande wa Malawi kwa maana hiyo mto wote ukawa upande waTanzania.

Ndugu Wananchi;
Katika kipengele cha Sita(Article VI) cha Mkataba huo, wakoloni hao walikubaliana kufanya marekebisho yampaka mahali po pote kama itakuwa ni lazima kufanya hivyo, kulingana namazingira na hali halisi ya mahali hapo. Kwa mujibu wa kutekeleza matakwa ya kipengele hicho mwaka 1898 Tume yaMipaka iliundwa. Ilianzia kazi katika MtoSongwe kuhakiki mpaka baina ya nchi yetu na Malawi. Tume ilikubaliana kuhamishampaka kutoka ufukweni mwa Mto Songwe upande wa Malawi na kuwa katikati yamto. Baada ya uhakiki katika eneo hilokukamilika, mwaka 1901 mkataba mpya ulisainiwa kuhusu mpaka huo.
Tume iliendelea na kazi yake katika ZiwaTanganyika na kuhamisha mpaka kutoka ufukweni hadi katikati ya ziwa na mkatabampya kusainiwa mwaka 1910. Tume iliendeleakatika ziwa Jipe ambapo mpaka ulihamishwa pia hadi katikati ya ziwa.

Ndugu Wananchi;Bahati mbaya Tume hiyohaikufanikiwa kufanya uhakiki wa mpaka katika Ziwa Nyasa kutokana na kutokeakwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kati ya mwaka 1914 - 1918. Kama tunavyokumbuka, Waingereza na Wajerumaniwaligeuka kuwa maadui na kupigana hata hapa nchini. Baada ya vita hivyo na Ujerumani kushindwa, Barazala Umoja wa Mataifa (The League of Nations) liliikabidhi Uingereza udhamini wa Tanganyika.Hivyo, Uingereza ikawa inatawala Malawi na Tanganyika.

Ndugu Wananchi;
Wakati Tume ya Uingereza naUjerumani ilipokuwa imekufa, Tume ya Mipaka kati ya Uingereza na Urenoiliendelea na kazi. Matokeo yake, mwaka1954, Uingereza na Ureno zilitengua mkataba wao wa mwaka 1891 ulioweka mpaka waZiwa Nyasa katika ufukwe wa mashariki ya Ziwa, yaani kwenye ufukwe wa Msumbiji,na kuuhamishia katikati ya ziwa.

Ndugu Wananchi;
Jambo la kustaajabisha ni kuwa,Waingereza walioona umuhimu na busara ya kurekebisha mpaka kati ya Malawi naMsumbiji, hawakuona umuhimu wa kufanya hivyo kati ya nchi yetu na Malawi. Inashangaza, kwa sababu wakati huo Uingerezailikuwa mtawala wa nchi zetu mbili hivyo kazi ya marekebisho ingekuwa rahisi,lakini hawakufanya hivyo. Na, baya zaidini kuwa hata pale watu wa nchi yetu walipotakakupatiwa ufafanuzi na kutaka ukweli uwekwe wazi kuhusu mpaka hawakusikilizwa. Watu walitaka ufafanuzi kwa sababuinasemekana kati ya mwaka 1925 na 1938, taarifa ya Uingereza kwa Umoja wa Mataifaziliweka mpaka katikati ya ziwa. Lakini,kuanzia mwaka 1948 mpaka ukawekwa tena ufukweni.

Ndugu Wananchi;
Mwaka 1959, 1960 na 1962, suala lampaka wa Malawi lilijitokeza tena na kujadiliwa na Bunge la Tanganyika, wakatiule lilijulikana kuwa Baraza la Kutunga Sheria, (Legislative Council – LEGCO). Hoja ya Wabunge wa Tanganyika ilikuwa kwamba mpakakuwekwa kwenye ufukwe wetu kunawanyima wananchi wa Tanganyika wanaoishi kandokando ya ziwa haki yao ya msingi ya kutumia maji kwa kunywa, kuoga, kuvua samakina kupata manufaa mengine yatokanayo na ziwa bila ya kuomba ridhaa ya Serikaliya Koloni la Nyasaland kama Malawi ilivyokuwa inajulikana wakati ule. Hoja iliyotolewa ilikuwa kwamba Serikali yaTanganyika ijadiliane na Serikali ya Nyasaland kupitia Serikali ya Malkia waUingereza ili ufumbuzi upatikane. Wakolonihawakujali na wala hakuna hatua zilizochukuliwa mpaka Tanganyika ikapata uhuruwake tarehe 9 Desemba, 1961 na Malawi kupata uhuru wake mwaka 1964.
Juhudiza Kubadili Mpaka wa Ziwa Nyasa Baada ya Uhuru
NduguWananchi;
Wakatitulipopata Uhuru mwaka 1961, mjadala kuhusu mpaka wa Tanganyika na Malawiuliendelea Bungeni, ambapo ilitolewa hoja kwamba zifanyike juhudi za makusudiza kuanzisha na kuendeleza mazungumzo ya kurekebisha mpaka huo kwa manufaa yawananchi wote wanaoishi pembezoni mwa ziwa. Iliamuliwa kwamba tusubiri mpaka wenzetu wa Malawi wapate uhuru ili yafanyikemazungumzo baina ya nchi mbili huru. Kulijengeka matumaini kuwa mambo yangekuwa rahisi. Bahati mbaya haikuwa hivyo na kwamba mamboyakageuka na kuwa magumu na ya uhasama. Miakamitatu baada ya Malawi kupata Uhuru wake (1964), kunako tarehe 3 Januari 1967,Serikali ya Tanzania iliandika barua kwa Serikali ya Malawi kuelezea tatizo la mpakawa ziwani na kupendekeza nchi zetu mbili zizungumze na kulitafutiaufumbuzi.

Ndugu Wananchi;
Bahati nzuri tarehe 24 Januari,1967, Serikali ya Malawi ikajibu kukiri kupokea barua hiyo na kuahidi kuwa itatoamajibu baada ya muda si mrefu. Hatahivyo, tarehe 27 Juni, 1967, Rais Kamuzu Banda akilihutubia Bunge la Malawi, alikataamaombi ya Tanzania. Alisema hayanamsingi na alidai kuwa kihistoria Songea, Mbeya na Njombe ni sehemu yaMalawi. Hivyo basi, mazungumzo yakafa.

Tanzania haikukata tamaa. Alipochaguliwa Rais wa Pili wa Malawi, MheshimiwaBakili Muluzi, juhudi zilifanyika lakini nazo hazikufika mbali. Bahati nzuritarehe 9 Juni, 2005, Rais wa Tatu wa Malawi, Mheshimiwa Bingu Wa Mutharika,ambaye sasa ni marehemu, alimuandikia barua aliyekuwa Rais wa nchi yetu wakatiule, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kushauri nchi zetu zifanye mazungumzokuhusu mpaka wa ziwani. Alipendekeza iundweTume ya Pamoja itakayojumuisha Mawaziri na Wataalamu kutoka nchi zetumbili. Tume hiyo itatoa mapendekezo kwaMarais wa nchi zetu mbili ambayo yatakuwa msingi wa majadiliano baina yao. Alisisitiza umuhimu wa kulipatia ufumbuzisuala hilo.

Ndugu Wananchi;
Kwa kuwa ilikuwa kipindi champito kuelekea kuchaguliwa Serikali ya Awamu ya Nne, Rais Benjamin Mkapahakuwahi kuishughulikia barua hiyo. Nilipoletewa barua hiyo nikaijibu kukubaliushauri na mapendekezo yake. Aidha, nilipendekezaWizara na Idara zipi za Serikali zetu zishirikishwe katika Tume hiyo. Bahati nzuri Rais wa Malawi alikubalimapendekezo yangu pamoja na lile la kwamba Malawi waitishe mkutano wa kwanza waTume hiyo.

Ndugu Wananchi;
Mpaka sasa mikutano mitatu ya Tumeya Pamoja imeshafanyika, wa kwanza ulifanyika tarehe 8 – 10 Septemba,2010. Mkutano wa pili ukafanyika tarehe27 – 28 Julai, 2012 hapa Dar es Salaam na wa tatu ukafanyika Mzuzu na Lilongwetarehe 20 – 27 Agosti, 2012. Hatua kadhaa zimepigwa lakini bado muafakahaujapatikana kwa maana ya madai yetu ya kutaka mpaka uwe katikati ya ziwa namadai yao kuwa mpaka ubaki ufukweni kwetu kama ilivyo kwenye Mkataba wa Heligoland wa Julai1, 1890. Hoja ya wenzetu ni kuwa huondiyo mpaka tuliorithi wakati wa uhuru. Wanataka tuthibitishe hivyo na kwamba tuzingatie kauli ya OAU yakuheshimu mipaka tuliyorithi kwa wakoloni. Wananukuu kauli ya Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere akisisitiza hoja hiyo katika mkutano wa OAU mwaka1963.
Hojaza Msingi za Kutaka Mpaka Uwe Katikati ya Ziwa
NduguWananchi;
Kwa upande wetu tumekuwa na hojakadhaa za kutaka mpaka uwe katikati ya ziwa. Ya msingi kabisa ni ukweli kwamba Mkataba wa Heligoland umekosewa kwakuamua kuwanyima wananchi wa Tanzania wanaoishi ufukweni mwa ziwa haki yao yamsingi ya kutumia maji na rasilimali zilizomo katika Ziwa Nyasa. Zipo sababu kadhaa kwa upande wetu kudaihivyo. Mojawapo ni sheria ya kimataifa inayoelekezakwamba po pote kwenye maji ya asili kama vile ziwa na mito iliyopo kati ya nchimbili mpaka huwa katikati. Ndiyoutaratibu unaotumika duniani kote, na mifano iko tele. Kwa nini iwe tofauti katika ziwa Nyasa na kwaupande wa Tanzania tu wakati kwa upande wa Msumbiji mpaka upo katikati ya ziwa?

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Mto Songwe, mpakabaina ya nchi zetu mbili upo katikati. Iwejehapa kanuni hiyo itambulike na kuheshimiwa lakini isiwe hivyo ziwani? Kama nilivyoeleza awali, mwanzoni Mto Songwe woteulikuwa umewekwa upande wetu, lakini Tume ya Mipaka iliyoundwa mwaka 1898ilifanya marekebisho na kuweka mpaka katikati ya mto. Kama nilivyokwishagusia kwenye ziwa hilo hilola Nyasa kwa upande wa Msumbiji mwaka 1954 mkataba wa mwaka 1891 ulioipa Malawiziwa lote ulirekebishwa na mpaka kuwekwa katikati. Kwa nini isifanyike hivyo hivyo kwa upande waTanzania? Hivi hasa ni kipi ambachowenzetu wa Msumbiji walichotuzidi na kustahili kupata haki yao ya msingi ya kumilikina kutumia maji ya Ziwa Nyasa ambacho sisi Tanzania tumepungukiwa?

Ndugu Wananchi;
Maji ni zawadi ya Mwenyezi Mungukwa wanadamu wake, waitumie kwa uhai na maendeleo yao. Iweje leo, kwa watu wanaoishi pembeni mwaziwa hilo hilo wengine wapewe na wengine wanyimwe haki ya kulimiliki na kulitumia?Kwa nini wanyimwe haki ya kunufaika na zawadi hiyo? Hivi kauli ya wakoloniwaliokaa Berlin ya kusema fulani apate na fulani asipate inatosha? Hivi kweli ni rahisi kiasi hicho?

Mpaka wa kwenye maji ni tofautina ule wa nchi kavu. Huu una rasilimaliambayo huwezi kuamua kumnyima mwanadamu mwingine anayeishi pembeni yake kwavile haina badala yake. Unapowaambiawatu wa Mbamba Bay, Liuli, Lituhi, Manda, Ngonga, Matema, Mwaya, Itungi nawengineo waishio kando ya ziwa kuwa maji hayo si yao bali ni mali ya Malawihawakuelewi na watakushangaa sana. Watadhani umechanganyikiwa kwani tangu waumbwe wamekuwepo hapowanamiliki na kutumia maji ya Ziwa. Unatakawafanyeje? Waende Malawi kuomba kibalicha kuyatumia? Wao watakuuliza swalimoja tu “hivi hao wenzao wanaoishi ng’ambo ya pili wamewazidi nini katikaubinadamu wao hata wapewe maji yote na wao wanyimwe?”

Ndugu Wananchi;
Kwa maana halisi ya Mkataba waHeligoland tangu tarehe 1 Julai, 1890, wananchi wa upande wa Tanzania wamekuwawanakunywa, kuoga, kuvua samaki na kusafiri katika maji ya Ziwa yasiyokuwa yaobali ya nchi nyingine. Na kwa kuwa wamekuwawanafanya hivyo bila ya kupata kibali cha Malawi wamekuwa wanaiba maji nasamaki wa Malawi na kusafiri isivyo halali katika nchi ya watu. Jambo hili haliingii akilini hata kidogo. Ndiyo maana tunadai haki yetu stahili.

Ndugu Wananchi;
Na hiyo pia, ndiyo maana, busara na hekima ya Sheria ya Kimataifa kuhusumpaka wa kwenye maji kuwakatikati. Sheria hii inazingatia halihalisi ya maisha ya jamii inayozunguka ziwa ambayo imekuwa inalitegemea maishayao yote kwa shughuli zao za kuwapatia uhai na maendeleo yao. Haiwezekani kuwatenganisha watu waishio kandoya Ziwa Nyasa kumiliki na kutumia maji hayo na rasilimali zake. Hawataelewa wala kukubali kuambiwa kuwa wanatumiamaji na rasilimali za ziwani kwa hisaniya nchi ya Malawi.

Kwa watu waliokuwepo tangu Mungu anawaumbawao na wenzao wa ng’ambo ya pili, siyo sawa na siyo haki hata kidogo kuwafanyiahivyo. Kwe kweli ni unyanyasaji wa haliya juu. Ndiyo maana wazee wetu walidaisuala hili liwekwe sawa wakati wa ukoloni, kabla na baada ya Uhuru. Na ndiyo maana na sisi tunafuata nyayo zaokatika madai haya ya haki.

Ndugu Wananchi;
Kuna mambo mengine mawili ambayo yanatufanyatudai haki ya kumiliki na kutumia Ziwa Nyasa. La kwanza ni ule ukweli kwamba mito mingi ya Tanzania nayo inachangiakujaza maji katika ziwa. Iweje leo maji yanayojazaziwa ni jambo jema, lakini yakishaingia ziwani, ziwa hilo si mali yao wenyemito hiyo tena na wakiyatumia wanaiba mali ya watu wengine. Hivi kwelindivyo wanavyostahili kufanyiwa watu wanaotunza vyanzo vya mito hiyo na kuruhusumaji yake kutiririka na kuingia ziwani?

Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ni kwamba mpaka waTanzania na Malawi kuwa ufukweni kunafanya ukubwa wa nchi zetu kuwa haujulikanikwa uhakika. Unategemea mabadiliko kutokanana kujaa na kupungua kwa majiziwani. Kunafanya mpaka wa nchi kuwahautabiriki na unaweza kuwa tatizo siku moja mbele ya safari. Isitoshe kuwa na nchi isiyojulikana ukubwawake nalo ni tatizo la aina yake. Ndiyomaana mpaka kuwa katikati ya ziwa ni bora zaidi.

Ndugu Wananchi;
Kama nilivyokwishasema, chimbukola mzozo huu ni mkataba wa Heligoland ambao umepanda mbegu ya fitina baina yanchi zetu. Bahati mbaya sana Tume yaMipaka haikumaliza kazi ya kuhakiki mipaka yote ya nchi yetu na majirani zake kufuatiakuzuka kwa Vita Kuu ya Kwanza mwaka 1914. Ujerumani ikashindwa vita na koloni lake kuwa sehemu ya himaya yaUingereza. Bahati mbaya kwetu Waingerezawaliotawala nchi zetu mbili tangu 1918 hawakuchukua hatua za kurekebisha mpakakabla ya uhuru wa nchi zetu. Ni maoni yetukuwa nchi zetu sasa zifanye kile ambacho hakikufanywa na Tume ya Mipaka ya wakoloni– Waingereza na Wajerumani. Tukifanyesisi wenyewe kama nchi mbili huru kwa njia ya mazungumzo.
Bahati mbaya majaribio ya mwaka1967 hayakufanikiwa. Bahati nzurikufuatia uamuzi wa kijasiri wa marehemu Rais Bingu wa Mutharika nchi zetu sasa zinazungumza. Bado hatujafikia muafaka kuhusu kurekebishampaka na huenda ikatuwia vigumu kufikia muafaka. Jambo linaloleta faraja, hata hivyo, ni kuwasote wawili tumekubaliana kuwa tutafute mtu wa kutusuluhisha.

Ndugu Wananchi;
Hayo ndiyo matokeo ya mazungumzoya Tume yetu ya pamoja tangu ngazi ya Wataalamu, Makatibu Wakuu mpaka kwaMawaziri, katika vikao vya Mzuzu na Lilongwe kati ya tarehe 20 – 27 Agosti,2012. Katika mkutano wao wa tarehe 27Agosti, 2012 Mawaziri husika wa nchi zetu chini ya uongozi wa pamoja wa Waziriwa Mambo ya Nje wa Malawi, Mheshimiwa Ephraim Chiume na mwenzake wa Tanzania,Mheshimiwa Bernard Membe, wameafiki mapendekezo hayo. Aidha, wamekubaliana kuwa pande zote mbiliwakutane tena Dar es Salaam kati ya tarehe 10 – 15 Septemba, 2012 kukubalianajuu ya usuluhishi wa aina gani unafaa.

Ndugu Wananchi;
Mtakubaliana nami kuwa tumepiga hatua muhimukuelekea kwenye kupata ufumbuzi wa kudumu wa suala hili. Hata hivyo, bado safari ni ndefu na huendaikawa na magumu mengi. Maombi yangu kwa viongozina wananchi wa Tanzania na Malawi ni kuendelea kuunga mkono jitihada hizi. Tuwaunge mkono wataalamu na Mawaziri wetu iliwafanikishe vizuri jukumu lao. Tuzingatie na kuheshimu walichokubaliana Lilongwe kuwa viongozi nawananchi wa nchi zetu wajiepushe na kutoa kauli au kufanya vitendo vinavyoweza kuchafuahali ya hewa, kuleta uchochezi na kuathiri majadiliano yanayoendelea.
Nawasihi Watanzania wenzangu kuzingatiaushauri na rai hiyo ya Mawaziri na wataalamu wetu, ili kuwe na mazingira mazuriya mazungumzo na kuwezesha mzozo huu kuisha kwa amani na kirafiki.
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napendakusisitiza kuwa si makusudio yangu wala ya Serikali yetu kutafuta suluhisho lasuala hili kwa nguvu ya kijeshi. NawahakikishiaWatanzania wenzangu kuwa hatuko vitani na Malawi na wala hakuna maandalizi ya vitadhidi ya jirani zetu hawa kwa sababu ya mzozo wetu wa mpaka katika Ziwa. Ondoeni hofu na endeleeni na shughuli zenu zaujenzi wa taifa letu kama kawaida.

Nilimhakikishia hivyo Rais waMalawi, Mheshimiwa Joyce Banda nilipokutana naye Maputo, Msumbiji tarehe 18Agosti, 2012. Tanzania haina mpango wakuingia vitani na Malawi. Mimi nawenzangu Serikalini tunaona kuwa fursa tuliyoitafuta miaka mingi ya kukaa nandugu zetu Malawi kuzungumzia suala hili lenye maslahi kwetu sote sasatumeipata. Hatuna budi kuitumiaipasavyo. Naamini, tukifanya hivyo,inaweza kutufikisha pale tunapopataka. Ni muhimu, kwa ajili hiyo kwa pande zetumbili, kuipa fursa ya mazungumzo nafasi ya kuendelea bila ya vikwazovisivyokuwa vya lazima.

Ndugu Wananchi;
Kwasababu hiyo basi , napenda kutumia nafasi hii kuwasihi ndugu zetu wa vyombo vyahabari na wanasiasa wenzangu tuepuke kauli au matendo yatakayovuruga mazungumzona kuchochea uhasama kati ya nchi zetu mbili jirani na rafiki. Kuna manufaa makubwa ya kumaliza mzozo wetukwa njia ya mazungumzo kuliko kwa njia ya vita. Kufikiria sasa kutumia njia nyinginezo hasa za nguvu za kujeshi, siwakati wake muafaka. Aidha, tukitumianjia ya vita, badala ya kuwa tumepata suluhisho inaweza kuwa ndiyo mwanzo wamgogoro mpana zaidi. Tuendelee kuwaungamkono wawakilishi wetu katika Tume yetu ya pamoja. Naahidi, Serikali itakuwa inawapa taarifakadri mazungumzo yetu na wenzetu wa Malawi yatakavyokuwa yanaendelea. Nina hakika tutamaliza salama.
MunguIbariki Tanzania!

MunguIbariki Afrika!

Asantenikwa Kunisikiliza

BARUA YA WAZI KWA RAIS WA DOLA YA ZANZIBAR DR. ALI MUHAMMED SHEIN

BISMILLAHI ‘RRAHMANI ‘RRAHIM

Kila sifa njema zinamstahikia Allah, Subhanah wa Taala, isofichika kwake dhulma wala harudishi dua ya mwenye kudhulumiwa. Rehma na amani zimshukie Mtume Muhmmad (s.a.w) kipenzi chake na cha umma, mtetezi wa waliodhulimiwa hata kabla ya kupewa Utume.

Mhishimiwa Rais,

Kwa mapenzi makubwa, baada ya kuisoma kwa utulivu khutuba yako ya siku tukufu ya Iddil Alfitri, nimelazimika kuandika barua hii kufuatana na kauli mbiu ya Mtume Muhammad (s.a.w) inayosema:

“…Dini ni nasaha…nasaha kwa Allah (S.w.T) na ni nasaha kwa Mtume (s.a.w.) na kwa viongozi wa Waislamu na kwa watu wote…”

Mh. Rais;
Ni kweli nchi yeti ya Zanzibar imechafuliwa jina lake kuwa ni nchi ya amani kama ilivyogeuzwa nchi yetu na ndugu zetu na kufanywa kuwa ni koloni lao baada ya mkoloni Mwingereza kutupa uhuru mwaka 1963 na kuwa na kiti chetu Umoja wa Mataifa huku walimwengu wote wakishuhudia; kiti ambacho kwa uwezo wake Allah atakirejesha karibuni na wewe ukiwa rais wa Zanzibar au uliyemwakilisha kuweza kuketi juu yake Insha’allah na sisi wananchi wako wa Zanzibar tukifurahikia jambo hilo adhimu.

Mh.Rais;
Ni kweli nchi yetu inatiwa dosari lakini si kweli kuwa wananchi wa Zanzibar ndio wanaosababisha dosari hiyo na doa hilo la uvunjifu wa amani; ushahidi wa maneno haya tutaupata tukirejea na kutizama kwa jicho la uadilifu na insafu katika matukio tafauti. Kwa hakika tukifanya hivyo tutagundua bila ya taabu kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania ndio wahusika wakuu na waanzilishi wa vurugu na uvunjifu wa amani ya nchi yetu ya Zanzibar kwa mara zote tatu, nikimaanisha machafuko yaliyotokea tarehe 25-26/5/2012 mjini Zanzibar na yale ya kuhujumu waumini na kunajisi misiskiti tarehe 17/6/2012, Donge, Mahonda na Mkokotoni pamoja na hujuma ya tarehe 20/7/2012 msikitini pia dhidi ya Waislamu walokusanyika msikiti wa Mbuyuni kuwasalia ndugu zao waliofariki kwa ajali ya meli ya Mv. Skaget. Waislamu tulihujumiwa ndani ya msikiti. Jeshi la polisi halikusita hapo bali liliwaingilia wananchi wanyonge mpaka ndani ya nyumba zao na kuwatendea matendo haramiya ya chuki na uhuni na katika waliotendewa matendo hayo maovu walikuwa wanawake na watoto wachanga. Polisi hao wakhalifu wa sharia waharibifu wa amani walifika hadi ya kutupa mabomu ya madawa makali ndani ya majumba ya raia bila ya kujali athari zitakazowasibu watoto wachanga na wanawake wenye kunyonyesha. Iwapo jeshi la polisi lililopewa jukumu la kulinda sharia, kuweka amani na kuwahami wananchi na mali zao ndio wenye kuvunja shariakwa kuwahujumu watu bila ya sababu, wananchi na haki zao zitalindwa na nani?

Mh.Rais;
Matokeo ya ukiukwaji wa sharia na haki za binadamu yaliyopelekea kuiharibia nchi yetu ya Zanzibar sifa yake ya amani na utulivu yamesababishwa na jeshi la polisi la Tanzania lililoacha kutekeleza wajibu wake wa kutunza amani ya nchi yetu Zanzibar . La kusikitisha zaidi ni kuwepo baadhi ya watendaji wako wa karibu wanaopotosha ukweli na kuifanyia khiyana nchi yetu ya Zanzibar kwa kufikisha kwako taarifa za uongo zilizopelekea kuitia doa na kuiharibu khutuba yako ilojaa maneno matukufu ya Allah Subhanah wa Taala pamoja na mafunzo kutoka Sunna za Mtume (s.a.w), khutuba ambayo ilitarajiwa kukemea dhulma za jeshi la polisi dhidi ya Waiislam na nyumba tukufu za Allah (S.w.T) iliyohujumiwa pamoja na wanawake na watoto wachanga ndani ya majumba kama ulivotetea makanisa na kubainisha hatari na ubaya wa walioyachoma makanisa hayo kwa lengo la kutaka kuanzisha fitna baina ya Waislam na jirani zao Wakristo waliokaribishwa nchini Zanzibar na kuishi pamoja nao miaka mingi kwa amani kiasi ambacho haijawahi kutokea Muislamu kulitusi kanisa licha kulichoma moto, kwani hayo ni kinyume na mafunzo ya dini yetu tukufu ya Kiislamu.

Mh.Rais;
Watu wanaokuwa karibu na Rais ni watu muhimu sana katika kufanikisha dhana ya uadilifu na utawala bora na wa haki usioogopa kukemea maovu hata kama walotenda au kuteleza ni Jeshi la Polisi kwani pia wao ni binaadamu siajabu kutenda makosa kwa maksudi seuze kuteleza, Allah Sbhanah wa Taala anatwambia: “…Enyi mloamini kuweni wasimamizi wa Allah wenye kushuhudia ukweli hata kama ni dhidi ya nafsi zenu…” Kwa hivyo, kosa kubwa zaidi ni kuuficha ukweli au kumpotosha kiongozi wa nchi hadi kufikia kuwashushia sifa wasiostahiki, wahuni ambao waliwatendea ya uhuni na dhulma kubwa hata wanawake na watoto. Ni khatari wadhulumiwa wanapofikishwa kumshtakia Mfalme wa Mbingu na Ardhi juu ya dhulma wanazotendewa. Isitoshe, khiyana ya watu kamaa hao wa karibu na viongozi kila inapojikariri khiyana hiyo inajenga hisiya kwa wenyeji wa nchi hii ambao wengi wao ni Waislamu kuwa wanabaguliwa, na sio wao tu bali hata kudharauliwa nyumba zao tukufu za ibada na kuthaminiwa makanisa peke yake. Sisi Waislamu hatutaki nyumba zozote za ibada zidharauliwe. Nyumba zote za ibada lazima ziwekewe hishima zinazostahiki.

Mh.Rais;
Kwa heshma zote naomba zichunguzwe sana sifa mbili kwa watu wote wa karibu na viongozi, sifa mbazo ni hatari kuzikosa tena zinaweza kuiangamiza nchi yetu tukufu ya Zanzibar . Sifa hizo si nyengine illa ni ukweli na uaminifu ambazo ni kinyume na uwongo na khiyana.

Yarabbi Muumba Mbingu na Ardhi, usieshindwa na jambo, tunakuomba muhifadhi Rais wetu, turejeshee nchi yetu kwa salama na amani, DOLA HURU YA ZANZIBAR, wastiri wanawake na watoto wachanga majumbani na Wazanzibari wote tunaodhulumiwa kwa kudai uhuru wa nchi yetu ya Zanzibar uloporwa na jirani zetu, ndugu zetu baada ya kutoka kwa wakoloni.

Amir Mkuu, Jumuiya ya Maimamu Zanzibar
Farid Hadi Ahmed

TGNP YALAANI KAULI ZA DC WA KOROGWE

DC Korogwe awajibishwe kwa udhalilishaji

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), tumesikitishwa sana na kauli iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Ndugu Mrisho Gambo, kwa mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bi. Najum Tekka, kuhusu uhalali wa shahada aliyonayo hususan kuihusisha shahada hiyo na vitendo vya ngono! Kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari ikiwepo gazeti la Majira Augosti 29,2012 Uk.3

Kauli hii ni udhalilishaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za wanawake na inaenda kinyume na misingi ya kuzingatia usawa sanjari na Katiba ya nchi ; Uwezeshaji wa wanawake na utekelezaji wa Maazimio ya Haki na Usawa katika ngazi za Kimataifa Kikanda na Nchini Tanzania.

Aidha kauli hii, inalenga kupotosha na kukatisha tamaa juhudi kubwa wanazofanya wanawake na wasichana katika kupata elimu na mafanikio mbalimbali nchini Tanzania. Zaidi ya hapo, kauli hii inadhalilisha na kushusha hadhi ya vyuo vya elimu ya juu vinavyofanya kazi kubwa ya kutoa elimu kwa Watanzania.

Kutokana na kauli hiyo DC amekiuka maadili ya uongozi wa umma na kukidhalilisha kiti cha ukuu wa wilaya na kiongozi Mkuu wa nchi aliyemteua kushika wadhifa huo. Aidha kauli ya kiongozi huyo ya kutimia mahakama kutetea hoja yake , kunaashiria ubabe , ujeuri, vitisho, kiburi na dharau ya kutaka kuingilia uhuru wa mahakama na ajenda binafsi isiyokuwa na maslahi kwa wanawake na umma wa Watanzania

Kutokana na kauli hiyo ya udhalilishwaji ,sisi wanaharakati wa ukombozi wa wanawake Kimapinduzi, usawa wa kijinsia, haki za kibinadamu demokrasia tunalaani vikali kauli za DC na kutoa Rai ifuatayo:

1. Mkuu wa Wilaya Ndugu Mrisho: amwombe radhi Mwanasheria Bi. Najum Tekka, kwa kosa la kumdhalilisha kijinsia

2. Tume ya maadili ya utumishi wa umma, na Mamlaka nyingine za kinidhamu zimchukulie hatua za kinidhamu Ndugu Gambo kwa kutumia lugha ya kudhalilisha watumishi kinyume na maadili.

3. Wanawake wote, wanaume, vijana wa kike na kiume kuendelea na mapambano dhidi ya mfumo dume na mifumo yote kandamizi, kushikamana katika kudai misingi ya kisheria, uwajibikaji inayozingatia usawa na haki na kukataa kudhalilishwa katika ngazi binasfi na za umma !.

Imetolewa
Dar es salaam leo 31/08/2012 na:
Usu Mallya
Mkrugenzi Mtendaji TGNP

Asenga Damian Abuubakar Mshindi nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wananfunzi wa vyuo vya elimu ya Juu nchini CCM, mkoa wa Dar es salaam Ndugu Asenga Damian Abuubakar, akibebwa juu juu na wapambe wake, baada ya kushinda nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa akiwakilisha wilaya ya Ifakara. Kijana huyo ambaye ni kada mkubwa wa Chama anawakilisha kundi kubwa la vijana wenye ari, uwezo na nia ya dhati ya kukisimamia Chama Cha Mapinduzi na kukiongezea nguvu na fikra mpya za Vijana ili kukijenga zaidi na kukiongezea ustawi.

SALAAM ZA SHUKURANI KWA WANA CCM DMV

Chama Cha Mapinduzi kinatoa shukurani za dhati kwa wanachama wake waishio maeneo ya Washington, DC , Maryland na Virginia kwa mchango wao wa hali na mali walioutoa katika kufanikisha sherehe hizi za ufunguzi wa Tawi.

Kwa kweli uongozi wa tawi umefarijika sana kuona wanachama wengi waliweza kuhudhuria sherehe hizo za ufunguzi wa tawi lao. Vile vile, sura hii imeonyesha namna gani chama cha mapinduzi ni chama bora kinachoweza kuwaunganisha wanachama wake popote duniani ili waweze kujiusisha na siasa ndani ya nchi yao. Hii ni fursa nyingine itakayowawezesha wanachama wa CCM kuchangia maoni bora yatakayowezesha kuimarisha chama na kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi wa nchi yao. Tunawasisitizia watanzania CCM ni chama tawala ambacho kina penda amani na utulivu sio chama cha vurugu na tunawahakikishia wanachama wote wa ccm muishi na watanzania wengine kwa upendo, amani na utulivu na kuweza kushirikaana na watanzania wenzetu katika mambo ya kila siku bila kujali tofauti za kisiasa. Sisi sote ni watanzania. Wana CCM tuwe mfano bora kwa jamii.

Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba:
1. Binadamu wake ni sawa bila kujali rangi, dini, kabila au maeneo aliyotokea mwanachama wake.
2. Kila mwananchi anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Kumshirikisha mwanachama kuchangia maoni yake ili kuimarisha sera na utekelezaji katika chama chake.

Amani , Upendo, Uzalendo na utaifa ni msisitizo mkubwa wa chama cha Mapinduzi kwa mtanzania popote alipo duniani. Sera hizi za CCM zimeifanya Tanzania kuwa kisiwa cha Amani na Utulivu barani Afrika.

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
ASANTENI SANA
Imetolewa na mwenyekiti wa tawi-DMV- Marekani
loveness Mamuya

CCM LONDON BARBEQUE OUTREACH PARTY 2012

---
Picha na -Maina Ang'iela Owino.

Mwenyekiti

Chama Cha Mapinduzi.

United Kingdom

Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal Akutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Dk. Mohammad Reza Rahimi Jijini Tehran

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Dk. Mohammad Reza Rahimi, walipokutana jana mjini Tehran na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano wa nchi zao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Serikali ya Tanzania uliohudhuri Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi za Siasa ya Kutofungamana na upande wowote uliomalizika jana mjini Tehran, Iran.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

SUPER D ATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA TAIFA

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' aliechuchumaa akiwa katika picha ya pamoja na mabondia wa Timu ya Taifa pamoja na Makocha wa timu hiyo alipotembelea mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea katika GYM ya Gymkhana kushoto ni Selemani Kidunda aliekuwa akituwakilisha katika mashindano ya Olimpic 2012 yaliyomalizika hivi karibuni wachezaji hawo kwa sasa wanajiandaa na mashindano ya Taifa yatakayoanza September 15 katika uwanja wa Ndani wa Taifa
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' wa pili kulia akiwa katika picha ya pamoja na mabondia wa timu ya taifa na makocha wenzake alipotembelea mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea katika GYM ya Gymkhana.

Wakazi wa Musoma Walivyodata Vilivyo na Ujio wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma, katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mmoja wa wasanii waliyoibuka kidedea katika mchakato wa Serengeti Super Nyota 2012, akidhihirisha uwezo wake wa kuimba ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Mwasiti akiwa amepakatwa na mmoja wa mashabiki zake kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma huku akiyamwaga mauno ya kiuchokozi chokozi.


Bofya hiyo video uone jinsi palivyokuwa hapatoshi ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lilipokuwa linaunguruma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoriki, akiwajibika mbele ya mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Ngosha the Swagadon, akiwaimbisha mashabiki (hawapo pichani) wake waliokuwa wamefurika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Wasanii wa Filamu Steve Nyerere (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana kuonesha uwezo wa kuzungusha mauno yao katika tamasha la Sererengeti Fiesta 2012, lililofanyika kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma.
Sehemu ya umati uliyofurika viwanjani hapo ukifuatilia kwa makini makamuzi ya wasanii hao wa Filamu, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Msanii mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma.
Kati ya mashabiki waliyoshindwa kujizuia katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, wakizungusha nyonga zao kama inavyoonekana kwenye viwanja vya Karume mjini Musoma.
Ray na Steve Nyerere (wa kwanza kutoka kushoto), wakishindana kusakata sebene kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Ray akipagawa na jukwaa huku makelele yakiwa yametawala kila kona uwanjani hapo.
Rais wa masharobaro Bongo, Bob Junior (katikati), akisongesha burudani za Serengeti Fiesta 2012, na Wanenguaji wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Profesa Jay akionesha uwezo wake wa kukamua jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Dimpoz na wanenguaji wake, wakiwajibika kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya viwanja vya Karume mjini Musoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Rachel (kushoto), akionyesha uwezo wake katika uwanja wa Karume mjini Musoma, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 na wanenguaji wake.
Rachel akikamua kwenye uwanja vya Karume mjini Musoma ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Chege,Temba na Bi Cheka wakiwajibika jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mashabiki wa kizungu wakipagawa na burudani ya Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini msoma.
Baadhi ya sehemu ya umati wa mashabiki waliozama ndani ya viwanja hivyo wakishuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Msanii wa michano ya Bongo Fleva, Nay wa Mitego akipagawisha jukwaani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Mmoja wa Ma'DJ wa Clouds TV, PQ akisababisha burudani ya Serengeti Fiesta 2012 mjini Musoma.
Mashabiki wa burudani za Serengeti Fiesta 2012, wakiwa wamefurika uwanjani hapo tayari kwa kushuhudia burudani mbalimbali.

Friday, August 31, 2012

Mjumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania inchini Afrika ya kusini Atembelea Tawil a CCM Afrika ya Kusini




Tony Blair in Malawi

President Banda welcomes Blair. Photo by Nyasa Times

President Banda gives Blair a gift. Photo by Nyasa Times

Blair addressing journalists with President Banda at Sanjika Palace. Photo Nyasa Times

17 WAWEKEWA PINGAMIZI USAJILI WA LIGI KUU TZ BARA

Klabu mbalimbali zimewasilisha pingamizi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupinga usajili wa wachezaji 17 walioombewa usajili katika timu za Ligi Kuu.

Toto Africans ya Mwanza imewawekea pingamizi wachezaji Enyinna Darlinton aliyeombewa usajili Kagera Sugar, na Mohamed Soud anayekwenda Coastal Union kwa maelezo kuwa bado ina mikataba na wachezaji hao.

Pia Flamingo ya Arusha inapinga usajili wa wachezaji wake Kelvin Friday Iddy katika timu za Azam na Salim Walii (Polisi Mara) kwa vile taratibu za kuwahamisha bado hazijafanywa. Nayo Kagera Sugar inapinga usajili wa beki David Charles Luhende kwenda Yanga kwa vile ada ya uhamisho haijalipwa.
Super Falcon ya Chanjamjawiri, Chakechake, Pemba inapinga wachezaji wake wanne; Edward Christopher Shija, Samir Said Luhava (Simba), Robert Joseph Mkhotya (African Lyon) na Sultan Juma Shija (Coastal Union) kusajiliwa katika timu hizo kwa maelezo taratibu halali za uhamisho hazikufuatwa.

Mchezaji Othman Hassan aliyeombewa usajili Coastal Union anapingwa na Oljoro JKT kwa vile bado ana mkataba na timu hiyo unaomalizika Mei 24, 2013. Nayo Rollingstone Multipurpose Ateclass Foundation ya Arusha inapinga usajili wa Kigi Makassy kutoka Yanga kwenda Simba hadi itakapolipwa fidia ya kumlea mchezaji huyo kwa vile bado hajafikisha umri wa miaka 23.

Azam inapinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba kwa maelezo bado ina mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani. Nayo Simba inapinga Kelvin Yondani kusajiliwa Yanga kwa maelezo kuwa ina mkataba naye uliosainiwa Desemba 23 mwaka jana.

Vilevile Simba imewasilisha malalamiko ya mchezo usio wa kiungwana katika usajili wa Mbuyu Twite aliyeko Yanga kwa maelezo alisaini mkataba na klabu yao Agosti Mosi mwaka huu mbele yao, viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na APR ambapo alilipwa dola 30,000 na nyingine 2,000 ikiwa ni fedha ya kujikimu na nauli yake ya kujiunga na klabu hiyo.

Nayo Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu Mbiyavanga na Lino Masombo kwa maelezo walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame. Pia inapinga Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam kwa msimu wa 2012/2013.

Pingamizi lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa kwa maelezo inao wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano. Imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia pingamizi hizo pamoja na usajili wa wachezaji kwa ujumla kwa 2012/2013.

TAMKO LA CHADEMA KUHUSU MAUAJI MKOANI MOROGORO

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapinga kauli za Serikali, Jeshi la Polisi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) zenye kulipotosha taifa kuhusu mashambulizi na mauji yanayoelezwa kufanywa na askari Mkoani Morogoro na badala yake kinataka uchunguzi huru ufanyike haraka kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act).

Kauli zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani zina mwelekeo wa kulilinda Jeshi la Polisi ambalo askari na maofisa wake ni sehemu ya watuhumiwa wa mauaji, badala ya kuwezesha ukweli kuthibitika na hatua kuchukuliwa kwa wahusika.

Hivyokutokana na kujirudiarudia kwa mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola CHADEMA kinatoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye kwa mujibu wa katiba ibara ya 33 ni mkuu wa nchi, kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu aingilie na kuwezesha uchunguzi wa kina.

Ikumbukwe kwamba tarehe 27 Agosti 2012 Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro lilifyatua risasi za moto na kupiga mabomu ya machozi wananchi na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamejikusanya kwa ajili ya kuelekea kwenye mkutano halali wa CHADEMA na wengine waliokuwa wakiendelea na shughuli zao eneo la Msamvu, hivyo kusababisha kifo cha raia mmoja asiye na hatia na kujeruhi wengine wawili.

CHADEMA kinaukumbusha umma kwamba kwa mauaji hayo na mengine katika maeneo mbalimbali nchini serikali inayoongozwa na CCM kupitia vyombo vya dola inaendelea kukiuka Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatambua kwamba uhai ni haki ya msingi kwa raia wote.

CHADEMA hakikubaliani na hatua zilizochukuliwa na Serikali mpaka sasa kuhusu tukio husika pamoja na maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani tarehe 28 Agosti 2012 ambayo kwa sehemu kubwa yametokana na taarifa zisizo za kweli kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Polisi ambao ni sehemu ya watuhumiwa wa mauaji husika.

CHADEMA haina imani na timu iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi kuchunguza tuhuma za askari kufyatua risasi na mabomu ya machozi na kusababisha mauaji kwa kuwa tayari serikali na Jeshi la Polisi wametoa maelezo yenye kutofautiana kwa kiwango kikubwa na maelezo ya mashuhuda waliokuwepo na ushahidi wa picha za eneo la tukio.

Wakati Serikali na Jeshi la Polisi wakitoa maelezo kuwa marehemu alikutwa umbali wa mita 300 na kupelekwa hospitali na wasamaria wema, mashuhuda wameeleza wazi kuwa askari walifika jirani na eneo lake na ofisa mmoja akaonyesha ishara na ndipo risasi za moto na mabomu ya machozi yakafyatuliwa mojawapo kumpata marehemu na kudondoka.

Mashuhuda wote waliohojiwa wanaeleza kwamba bunduki ya polisi ndiyo ilielekezwa na kufyatuliwa kwa marehemu, maelezo pekee yanayotofautiana ni kuwa baadhi wameeleza kuwa ni bunduki ya risasi za moto na wengine wa wameeleza kuwa ni bunduki ya kufyatulia mabomu ya machozi.

Mara baada ya kudondoka gari hilo liliondoka na gari lingine la polisi lilifika likiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia cha Mkoa ambaye alitoa amri ya gari lingine kumbeba Ali Hassan Singano (Zona) na kuondoka naye, hivyo si kweli kwamba matukio hayo yalitokea mbali na eneo bali pembeni ya meza ya muuza magazeti huyo karibu na barabara ya kwenda Iringa eneo ambalo polisi ilikuwa ikifanya mashambulizi.

Kauli zilizotolewa na Serikali kuwa Jeshi la Polisi lilizuia maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika Mkoani Morogoro kwa sababu ya sensa ya watu na makazi si za kweli kwa kuwa sababu pekee zilizotolewa ni ufinyu wa barabara na kuwa maandamano yalipangwa siku ya kazi. Ushahidi wa suala hili ni barua ya Jeshi la Polisi lenyewe ya 23 Agosti 2012 yenye Kumb. Na. MOR/A.25/1/VOL. II/202.

CHADEMA kinaujulisha umma kwamba Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro ndilo lililoacha kuheshimu utawala wa sheria na makubaliano yaliyofikiwa baada ya mazungumzo yaliyohusisha kikosi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kikiongozwa na Kamanda wa Operesheni za Jeshi hilo Simon Siro na hivyo kuwa chanzo cha mauaji yaliyotokea na madhara mengine kwa wananchi waliokuwepo maeneo yaliyorushiwa mabomu ya machozi.

Ikumbukwe kwamba awali CHADEMA kilipanga kufanya maandamano na mikutano katika Jimbo la Morogoro Mjini tarehe 4 Agosti 2012 na kuwasilisha taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, Polisi wakakataa kufanyika kwa maandamano na mikutano kwa kisingizio cha Sikukuu ya Nanenane, mgomo wa walimu na ratiba kugongana na ile ya mikutano ya CCM, sababu ambazo zilibainika kwamba hazikuwa na msingi wowote.

Baada ya mvutano na mazungumzo CHADEMA ilikubali kutii sheria na kuzingatia matakwa ya Jeshi la Polisi pamoja na kuwa yalitolewa kinyume cha Sheria kwamba maandamano na mkutano wa CHADEMA vifanyike mara baada ya siku ya kuanza kwa sensa tarehe 26 Agosti 2012 na CHADEMA ilipendekeza tarehe 27 Agosti 2012 ambayo Jeshi la Polisi liliikubali.

Polisi walifanya hivyo wakielewa ukubwa wa barabara za Morogoro na pia wakitambua kwamba ilikuwa ni siku ya kazi, hata hivyo tarehe 23 Agosti 2012 Jeshi la Polisi liliandika barua ya kueleza kwamba limetoa kibali cha mkutano (suala ambalo si mamlaka yake kisheria) na pia limekataza maandamano.

CHADEMA kikaamua kwa mara nyingine tena kurudi katika meza ya mazungumzo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, tarehe 24 Agosti 2012 ambapo polisi ilikubali maandamano ikiwemo ya watembea kwa miguu na kupendekeza njia mbadala na tarehe 26 Agosti 2012 mazungumzo yakaendelea kwa lengo la kukagua barabara.

Hata hivyo, kufuatia shinikizo la Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile kinyume na Sheria ya Jeshi la Polisi ambayo imetoa mamlaka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya kuhusu taarifa za mikutano, polisi ikarejea katika msimamo wa kukataza mapokezi ya watembea kwa miguu na badala yake tarehe 26 Agosti 2012 bila sababu za misingi ya kisheria na zisizozingatia haki za kikatiba ikapendekeza kwamba yafanyike mapokezi kwa kutumia magari.

Maelezo ya Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa iwapo vyama vya siasa visiporidhika na mazingira kama hayo yapo mamlaka ya kukata rufaa yanapotosha kwa kuwa Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Vyama vya Siasa hazijaweka utaratibu wa rufaa hivyo njia pekee ya kisheria ni kutumia mahakama.

Jeshi la Polisi lingeheshimu utawala wa sheria na mazungumzo lingeruhusu CHADEMA ifanye maandamano na kutoa ulinzi mpaka eneo la mkutano kwa muda mfupi badala yake jeshi hilo likaamua kutumia nguvu kubwa na kusababisha mauaji, barabara kufungwa kwa muda mrefu na kuathiri wananchi waliokuwa wakiendelea na kazi zao.

Iwapo wanachama na wananchi waliokuwa wamekusanyika kuwapokea viongozi na kuelekea kwenye mkutano wangekuwa wamekiuka sheria Jeshi la Polisi lingeweza kuwakamata kwa mujibu wa sheria, hata hivyo hakuna kiongozi yoyote wa CHADEMA aliyefunguliwa jalada mpaka sasa katika kituo chochote cha polisi kwa kudaiwa kukiuka sheria.

Kinyume chake Jeshi la Polisi ambalo likiwa kwenye mazungumzo lilikubali kuwa mapokezi yafanyike kwa msafara wa vyombo vya moto, lakini tarehe 27 Agosti 2012 likaamua kupiga mabomu ya machozi kwa wananchi na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamekusanyika eneo la Msamvu wakiwasubiri viongozi bila hata ya kusubiri kuona iwapo yangefanyika matembezi ya miguu kuelekea eneo la mkutano au maandamano ya magari na vyombo vingine vya usafiri.

Kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kinyume cha sheria na kusababisha mauaji na kufunga barabara kwa muda mrefu kiliwafanya wanachama wa CHADEMA na wananchi kwa ujumla kutawanyika kuelekea eneo la mkutano na wengine kuingia barabarani kutembea kuelekea eneo la mkutano na hatimaye polisi walipoona wamesababisha hali hiyo wakaamua kulinda misafara hiyo mpaka eneo la mkutano hali inayodhihirisha kuwa uamuzi kama huo ungechukuliwa kutoka mwanzo yasingetokea madhara yoyote.

Kwa kuzingatia utofauti mkubwa baina ya maelezo yanayotolewa na Serikali na Jeshi la Polisi kuhusu matukio husika na ukweli halisi ulivyotokea, CHADEMA kinasisitiza kuwauchunguzi huru ufanyike kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) Sura ya 24 ya Sheria za Tanzania.

CHADEMA kwa mara nyingine kinaitaka Serikali inayoongozwa na CCM kurejea katika kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchunguzi wa Vifo, ambacho kinatoa mamlaka ya Waziri mwenye dhamana na masuala ya Sheria kuanzisha Mahakama ya Kuchunguza Vifo hivyo (Coroner’s Court) katika maeneo ya serikali za mitaa kwa kushirikiana na Jaji Kiongozi.

CHADEMA kinaikumbusha Serikali kuwa, kufuatia kauli ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mawaziri Vivuli husika kueleza bungeni taarifa za mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola kwa nyakati mbalimbali, Waziri Mkuu na Mawaziri wengine waliahidi bungeni kwamba sheria hiyo itaanza kutumika kuchunguza vifo vyenye utata.

Katika muktadha huo uchunguzi wa kifo cha Ali Zona haupaswi kufanywa na timu ya polisi bali sheria hiyo sasa ianze kutumika.

Kwa upande mwingine, CHADEMA imeheshimu taratibu za maziko zilizopangwa na familia ambapo mwili wa marehemu ulisafirishwa jana tarehe 28 Agosti 2012 kwenda Mkoani Tanga kwa ajili ya maziko na CHADEMA kuwasilisha rambirambi zake za awali, taarifa zaidi kuhusu ushiriki kwa CHADEMA kwenye maziko zitaelezwa baada ya majadiliano yanayoendelea na familia.

CHADEMA kwa kuheshimu mazungumzo na utawala wa sheria kwa mara nyingine tena tarehe 28 Agosti 2012 CHADEMA kimesitisha Operesheni za Maandamano na Mikutano yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa rai iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ili kupisha kukamilika kwa zoezi la sensa ambayo imetokana pia na maelezo ya mamlaka zingine za kiserikali.

CHADEMA inatambua kwamba wakati maandamano ya CHADEMA yametolewa rai kuwa yasitishwe kupisha sensa, maandamano ya wagombea wa CCM kurudisha fomu za uchaguzi wa ndani ya chama chao yameachwa yakiendelea katika barabara kadhaa nchini bila kusitishwa kwa kisingizio hicho.

Aidha, wakati CHADEMA ikiheshimu mazungumzo na kusogeza ratiba yake mbele ya tarehe 26 Agosti 2012 mpaka tarehe 27 Agosti 2012 kupisha sensa hatua ambayo ilifanywa pia na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo ilitangaza ratiba yake kuendelea baaada ya tarehe hiyo.

Tume hiyo inaendelea na mikutano yake ya hadhara inayokutanisha wananchi katika kata za mikoa mbalimbali wakati huo huo zoezi la sensa likiendelea lakini kwa mikutano ya CHADEMA inaonekana kufanyika kwake ni kuingilia sensa.

CHADEMA inataka Serikali na Polisi kueleza iwapo matukio haya na mengine hayana mwelekeo wa ubaguzi na uhujumu wa vuguvuvugu la mabadiliko linaloendelea nchini kwa kurejea ukweli kuwa maisha ya wachache yanaweza kuwekwa mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.

CHADEMA itaeleza hatua za ziada itakazochukua baada ya kupata ripoti ya uchunguzi wa mwili wa marehemu (post mortem) uliofanyika tarehe 28 Agosti 2012 na uamuzi wa Serikali kukubali au kukataa mwito wa kutumia Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) kuwezesha uchunguzi huru.

Imetolewa
tarehe 29 Agosti 2012 na:
John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

Popular Posts