Pages

Friday, November 23, 2012

Statement by the Spokesperson of High Representative Catherine Ashton on the situation in Eastern Congo following the Communiqué of Kampala


Statement by the Spokesperson of High Representative Catherine Ashton on the situation in Eastern Congo following the Communiqué of Kampala

BRUSSELS, Kingdom of Belgium, November 23, 2012/African Press Organization (APO)/ – The spokesperson of Catherine Ashton, High Representative of the European Union for Foreign Affairs and Security Policy and Vice President of the Commission issued the following statement today:
“The High Representative would like to welcome the statement jointly endorsed by Presidents Museveni, Kagame and Kabila following their meeting in Kampala on the situation in Eastern Congo, convened by President Museveni in his capacity as chair of the International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR).
It is an important step forward to stop a further deterioration of the crisis and to start working on sustainable solutions.
The High Representative encourages all stakeholders to work in good faith in order to rapidly implement the agreement, starting with the immediate halt of the M23 offensive and its pull-out of Goma.
She calls on all parties to grant unhindered humanitarian access to those in need immediately.
The EU, in close coordination with the United .ations and other international partners, is ready to support the region in its efforts with a view to contributing to a sustainable solution for the crisis.”

Foreign Minister Westerwelle calls for end to military offensive by rebel group M23


BERLIN, Germany, November 23, 2012/African Press Organization (APO)/ Since 15 November, fighting has taken place in the Democratic Republic of the Congo between government troops (FARDC) and M23 rebels. The rebels have already taken Goma, the capital of North Kivu, and are now approaching Bukavu in South Kivu.
Federal Foreign Minister Guido Westerwelle expressed his concern over the situation and issued the following statement in Berlin today (22 November):
I have been following developments in the eastern part of the Democratic Republic of the Congo with increasing concern.
I welcome the fact that talks are now taking place between Presidents Kabila of the Congo, Kagame of Rwanda and Museveni of Uganda. Their aim must be to prevent military conflicts, end the violence in eastern Congo and find political solutions to the region’s many problems.
Building confidence and cooperating in earnest are – especially between Rwanda and the Democratic Republic of the Congo – the key to a sustainable solution. People are suffering, and if fighting were to break out again, their fate would be even worse. M23 must retreat from Goma, end its military offensive and respect the territorial integrity of the Democratic Republic of the Congo. Any further destabilization of eastern Congo must be prevented.
All parties are called upon to respect human rights and protect the civilian population.

SOURCE 
Germany – Ministry of Foreign Affairs

SAFARI LAGER KUZINDUA MSIMU WA PILI WA PROGRAMU YAWAJASIRIAMALI YA “SAFARI LAGER WEZESHWA” JIJINI MBEYA


Balozi wa Safari Lager Wezesha, Janeth Karabu(kushoto) akiwaelimisha wakazi wa Iringa Mjini kuhusu Safari Lager Wezeshwa awamu ya pili Mkoani hapo mwishoni mwa wiki.

Balozi wa Saafari Lager Wezesha, Sarafina Msawe(katikati) akiwaelimisha wakazi wa Iringamjini kuhusu programu ya Safari Lager Wezeshwa  awamu ya pili iliyozinduliwa mwinshoni mwa wiki Mkoani hapo.


KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager             leo inatarajia kuzindua rasmi msimu wa pili wa programu ya kuwaelimisha wajasiriamali wa jijini Mbeya juu ya “Safari Lager Wezeshwa”.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam jana Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema timu ya Mabalozi 15 wa ya kuelimija jamii imeshawasili jijini Mbeya tayari kuanza kutoa elimu kwa jamii ya wakazi wa Mbeya hasa wafanyabiashara ndogo ndogo na wa kati juu ya programu ya Safari Wezeshwa.
Alisema Shelukindo, timu hiyo ilianzia Mkoani Kilimanjaro,Arusha,Mwanza,Shinyanga,Morogoro,Iringa na Tanga ikielimisha jamii ya Watanzania juu ya programu hiyo na sasa leo ni jijini Mbeya ambapo watafanyakazi katika viwanja vya Malimbali vya jijini Mbeya kwa siku mbili wakielimisha jamii juu ya Safari Lager Wezesha  na baada ya hapo watahamia Mkoani Lindi na Mtwara.
Programu  hii ilipata mafanikio makubwa, mwaka jana iliwawezesha wajasiriamali 54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na ruzuku za vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili. Bwana Shelukindo alisema, “Safari Lager kwa mara ya pili  inawaletea wamiliki wa biashara nafasi ya kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa ruzuku nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika harakati za kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaoingia na kufuzu vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia hasa ya Safari Lager ni kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia mafanikio katika kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii inayowazunguka”.Alifafanua kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo wadogo na sio wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya programu hiini kutoa hamasa kwa wajasiriamali
kote Tanzania ili wajitahidi zaidi katika shughuli wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze kufikia ndoto zao. Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama fedha taslimu kwa watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi vitakavyomsadia mjasiriamali kulingana na kazi anayofanya.
Shelukindo alimaliza kwa kuwapa changamoto wajasiriamali kujitahidi zaidi sio tu kwa ajili ya kujishindia ruzuku za programu ya“Safari Lager Wezeshwa” lakini kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla. Aliwasihi wajasiriamali na wafanyabiashara kwa ujumla kutega sikio kwa taarifa zaidi juu ya usajili na kutembelea website yawww.wezeshwa.co.tz.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kusema, “Tunatoa pongezikwa wajasiriamali kote Tanzania, Safari Lager inatambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu. Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba waendelee kuburudika na bia hii inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio unaofanya tunawawezesha wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia kamili, inayodhihirisha mabingwa!.

KINANA ALIPOTUA KWA MUDA TABORA NA KUKUTANA NA VIONGOZI WA MKOA


 Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana, akimsalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa, wakati alipotua kwenye uwanja wa Ndege wa Mkoani humo leo asubuhi kwa ajili ya kukutana na baadhi ya Viongozi wa CCM wa mkoa huo. Wengine ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na  Seif Khatib, anayeshuka kwenye ngazi ndegeni ni Mwanri.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Tabora alipotua kwa muda mkoani humo wakati akitoka Rukwa kuelekea Geita asubuhi hii.
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akipotua kwa muda mkoani humo akitokea Rukwa kwenda Geita asubuhi hii.

MBEKI MGENI RASMI MAJADILIANO YA UONGOZI AFRIKA DAR ES SALAAM


 Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akifafania jambo wakati wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya. Mbeki alikuwa Mgeni Rasmi katika mdahalo huo.
 Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo, ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mdahalo huo jijini Dar es Salaam leo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja, akizungumza katika mdahalo huo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akikiwa mwenye tabasamu wakati Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akitoa ufafanuzi wa majadiliano.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya na Mwenyekiti wa Mdahalo wa Uongozi Afrika, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja (katikati) wakimsikiliza Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ami Mpungwe ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Tanzanite One muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Mgemi rasmi wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo. 
Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Tanzania, Cleo David Msuya (kulia)  na Salim Ahmed Salim wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA KOREA, NCHINI TANZANIA KWA MAZUNGUMZO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Korea nchini Tanzania, IL Chung, wakati alipofika ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Korea nchini Tanzania, IL Chung, mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.

Katibu Mkuu wa CCM Abdurahamn Kinana Atua Mkoani Rukwa na Kusema'' Kuitwa Waheshimiwa Ndani ya CCM Sasa Basi.''


Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahaman Kinana akifungua shina la wakereketwa wa CCM la Kisesa, mkoani Rukwa.
Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahamn Kinana,na Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye , na Mzee Self Khatib wakisalimia wananchi Uwanja wa Ndege wa Rukwa.
Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akiwa na Watoto
Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahaman Kinana akizungumza na wana-CCM leo mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa
Pikipiki za mapokezi kutoka Uwanja wa Ndege wa Rukwa.Picha na Bashir Nkromo-Rukwa
---
NA BASHIR NKOROMO, RUKWA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameagiza kuanzia sasa wanachama wa CCM kuacha kuitana waheshimiwa badala wake watumie jina ndugu kama alivyoasisi Mwenyekiti wa kwanza wa CCM, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Kinana ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na viongozi wa CCM, mjini hapa, akiwa katika siku yake ya pili ya ziara ya siku nne kujitambulisha na kukagua uhai wa Chama katika mkoa huo na mikoa ya Mtwara, Geita na Arusha.

"Mimi katika maisha yangu yote ya kumfahamu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, sikupata kumsikia akijiita au akitaka aitwe Mheshimiwa Mwenyekiti, au Mheshimiwa Rais, sasa haya mambo ya sisi kuitama mheshimiwa tunayatoa wapi?", alihoji Kinana.

Alisema, Mwalimu Nyerere hakujiita Mheshimiwa kwa sababu na maana kubwa sana, kwa hiyo ni lazima Wana-CCM kuendelea utamaduni huo wa kuitaka ndugu kwa sababu unazuia matabaka ya ubwana na utwana.

Mapema kabla ya mkutano huo wa ndani, Kinana alifungua shina la wakereketwa wa CCM Isesa na shina la UWT, Chanji nje kidogo ya mji wa Sumbawanga, ambapo alisema hatua ayake ya kufungua matawi hayo na kushiriki kikao cha shina kinachofunguliwa na mjumbe wa shina husika, ni ishara ya kuwaagiza viongozi wa ngazi zote wa CCM kuhakikisha wanatembelea mashina na matawi.

"Hili siyo langu, ni agizo la Mkutano Mkuu wa CCM uliomaizika mjini Dodoma hivi karibuni, pale tuliazimia kwamba, ili kuimarisha uhai wa Chama lazima viongozi wa ngazi mbalimbali watembelee mashina ma matawi ili kuzijua kero zilizopo huko", alisema.

Alisema, kulingana na agizo hilo, sasa kila kiongozi wa Chama atapimwa ufanisi wake wa kikazi kwa kuangalia ni namna gani anafanya kazi zake kwa karibu sana na mashina na matawi.

Alisema, CCM imesisitiza lifanyike hilo kwa juhudi zaidi kwa sababu ni wazi kwamba wenye chama ni wanachi waliopo kwenye ngazi hizo za mashina na matawi, hivyo kwenda huko ndiko kutaimarisha chama kwa uhakika zaidi.

Katika ziara hiyo, Kinana amefuatana na wajumbe wa NEC, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi), Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni)na waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri.

Mwisho.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba Yakusanya Maoni Tarime,Mara



Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphery Polepole (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa wananchi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo jana alhamisi Nov.22, 2012. Wajumbe wengine wa Tume, wa kwanza kulia Nassor Mohammed, Maria Kashonda na Riziki Ngwali.
Wananchi wa kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadlliko ya Katiba jana  alhamisi Nov. 22, 2012 katika kijiji hicho.
---
Na Ismail Ngayonga-Tarime, Mara

MKAZI wa Kata ya Kata ya Mliiba Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marco Magubo (31) amependekeza ni vyema Katiba Mpya ikataze vyama vya siasa vinavyoingia madarakani mara baada ya kushinda uchaguzi wa Rais visipeperushe bendera yake na badala yake kuweka bendera ya Taifa.

Akitoa maoni yake jana (Alhamisi Nov. 22, 2012) kuhusu Katiba Mpya kwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alisema kitendo cha kupeperusha bendera ya chama kilichoingia madarakani kitaongeza chuki kwa wanachama wa Chama kingine cha siasa kilichoshindwa uchaguzi.

Aidha Magubo alisema Rais anayeingia madarakani anawakilisha maslahi ya wananchi wote na hivyo si busara kwa Chama kilichoshida uchaguzi kupeperusha bendera ya Chama chao kwani Kiongozi huyo haongozi wanachama wa chama chake pekee bali wananchi wote katika taifa.

“Tazama Marekani ambao hivi majuzi tu walifanya uchaguzi mkuu wa Rais, katika kampeni za vyama vyao hatukuweza kuona bendera ya Republican wala Democracy ambavyo vyote vilishiriki uchaguzi na badala yake tuliona wananchi wakipeperusha bendera ya Taifa lao na hatukuona bendera ya Republican wala Democracy” alisema

Alisema kwa kuwa Tanzania ni nchi ya umoja, amani na mshikamano ni vyema  Katiba Mpya ikewe kipengele cha kukataza bendera za vyama vyao na badala ya wamwachie Kiongozi aliyopo madarakani kutetea hoja za wananchi wote.

Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana Aung'uruma Sumbawanga na Kuhudhuria Kikao Cha Shina


Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Chipukuizi wa CCM, wakati wa mapokezi yake kwenye Uwanja wa Ndege wa  Sumbawanga mkoani Rukwa, alipowasili mkoani Rukwa, jana, akiwa katika ziara yake ya siku nne kujitambulisha, kukagua na kueleza kwa wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika mkoa huo na mikoa ya Mtwara, Geita na Arusha.
Kinana akimsalimia aliyekuwa mbunge wa Sumbawanga mjini Hilary Aeshi, kwenye Uwanja wa Ndege wa  Sumbawanga mkoani Rukwa, jana.
Kinana akimsalimia Mwanasiasa mkongwe, Chrisant Mzindakaya, kwenye Uwanja wa Ndege wa sumbawanga, mkoani Rukwa, jana
Mjumbe wa Shina namba moja la Kisesa mkoani Ruwa,  Simoni Kibona akimsalimia kwa furaha, Kinana alipofika kwenye tawi hilo, jana na kushiriki kikao cha hilo ikiwa ni sehemu ya kuhimiza viongozi kutembelea mashina na matawi ya CCM ili kuimarisha chama.
Wajumbe wa mkutano wa shina namba moja la Kisesa mkoani Rukwa wakimsikiliza Kinana wakati akiwahutubia, aliposhiriki mkutano wao uliofanyika jana.
Kinana akifurahia ngoma ya kina mama wa shina la Isesa, mkoani Rukwa
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggry Mwanri  akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jana mjini Sumbawanga
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nape akihutubia  mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jana mjini Sumbawanga
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib akisalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Wananchi wakiwa na ujumbe wao kwenye bango katika mkutano wa CCM uliofanyika Sumbawanga mjini mkoani Rukwa jana.
Wana-CCM wakiwa na bango la kumpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdylrahman Kinana, mpongeza Kinana katika mkutano uliofanyika jana Sumbawanga mjini mkoani Rukwa.Picha na Bashir Nkromo-idara ya itikadi na Uenezi-CCM

Usu Mallya Awaasa Wananchi Kushiriki Kikamilifu Mchakato wa Katiba Mpya


Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Usu Mallya akizungumza katika tamasha hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Usu Mallya(kushoto) akiwa na mwenyeji wake Diwani wa Kata ya Mkambarani, Daniel Shawa (CCM)
Kutoka kushoto ni Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Usu Mallya  akiwa na Diwani wa Kata ya Mkambarani, Daniel Shawa (CCM) wakizungumza katika tamasha hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Usu Mallya akijumuika kucheza ngoma.
Mmoja wa wafanyakazi wa TGNP (kushoto aliyesimama) akiwezesha mada.
Mwezeshaji wa mada akizungumza kwenye mijadala ya vikundi.
Baadhi ya wananchi kwenye mkutano huo
--
Na Mwandishi wa Thehabari.com Morogoro

MKURUGENZI Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uundwaji wa Katiba mpya ili itakapo kamilika sera na sheria za nchi ziendane na wananchi wake, jambo ambalo litasaidia kutatua migogoro anuai.

Mkurugenzi huyo aliyasema hayo jana eneo la Mkambarani mje kidogo ya Mji wa Morogoro ambapo linafanyika tamasha la Jinsia katika ngazi ya wilaya lililoandaliwa na TGNP, kuchochea juhudi za wananchi hasa waliopo pembezoni kushiriki katika mchakato wa maendeleo yao.

Akizungumza katika mkutano huo unaowashirikisha wanavijiji kutoka baadhi ya vijiji vya Mkoa wa Morogoro na baadhi ya mikoa ambao ni wanaharakati wa ngazi za jamii, alisema ushiriki wa wananchi ipasavyo katika mchakato huo itasaidia mabadiliko ya mfumo wa uandaaji wa sera na sheria ili zisiendelee kulalamikiwa na wananchi.

“Mfumo uliopo sasa yawezekana kabisa ukawa na upungufu, ndio maana hata kwa sasa baadhi ya maeneo yanapata huduma za kijamii huku maeneo mengine yakilegalega kihuduma,” alisema.

Alitolea mfano eneo la Mkambarani wananchi wanalalamikia migogoro ya ardhi hali hiyo inachangiwa na mfumo katika mgawanyiko wa rasilimali ikiwemo ardhi, ambapo baadhi ya makundi yamekuwa yakisahaulika huku wajanja wakineemeka na mifumo hiyo.

Alisema wananchi wanapaswa kushirikishwa kwa karibu katika uandaaji wa sera na sheria na pia kushirikishwa kwenye mipango ya maendeleo ili kuondoa mkanganyiko ambao hujitokeza hapo baadaye. “Wananchi lazima tushirikishwe katika mipango ya maendeleo…tukumbuke kwamba hakuna sera na sheria inayonihusu mimi bila mimi kushirikishwa,” alisema Mallya.

Aidha aliwataka wanawake na wapenda mabadiliko kushiriki katika vuguvugu la kupambana na mfumo dume na kandamizi ambao kwa kiasi kikubwa unawaathiri akina mama. “Tukubali kuwa huu ni mchakato wa mabadiliko, tukatae uonevu na kupambana na mifumo yote kandamizi kwa kutumia umoja wetu pamoja na ushirikiano…umefika wakati wa kushirikiana katika masuala ya maendeleo, tusiishie kwenye harusi na misiba tu,” aliongeza.

Tamasha la jinsia ngazi ya wilaya linalofanyika nje kidogo ya mji wa morogoro linatarajiwa kumalizika leo jioni ambapo washiriki kwa pamoja watatoka na maadhimio ambayo yatafanyiwa kazi kulingana na maitaji.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com  

Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Alipotua Nchini Vietnam na Muendelezo wa Ziara Yake Nchini Humo



  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakipokea mashada ya mauwa kama ni Ishara ya ukaribisho katika Ikulu ya Vietnam,alipofika kwa mazungumzo na Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akiwatambulisha Viongozi aliofuatana nao kwa Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi,Nguyen Thi Doan,walipowasili Ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo,ya kuimarisha uhusiano na Ushirikiano baina ya pande zote, akiwa katika ziara rasmi ya wiki moja nchini humo.
  Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwamamwema Shein, akisalimiana na Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,alipowasili Ikulu nchini Vietnam,alipofuatana na Rais wa Zanzibar katika ziara Rasmi ya Kiserikali Nchini Vietnam ya wiki moja
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akisalimiana na Mawaziri na Viongozi mbali mbali wa Nchini Vietnam ,alipofika ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo na Makamo wa Rais Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akisalimiana na Makamo wa Rais Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,alipowasili Ikulu nchini Vietnam,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein,(katikati) akiwa ujumbe aliofuatana nao katika Mkutano maalum na Uongozi wa Serikali ya Vietnam,ukiongozwa na Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Bibi Nguyen Thi Doan,(hawapo pichani) katika ukumbi wa Ikulu ,katika kuimarisha Uhusiano na Ushirikiano baina ya pande mbili hizo,katika ziara rasmi ya Kiserikali.
Viongozi wa Serikali waliofuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakiwa kwenye mkutano maalum na uongozi wa serikali ya Vietnam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekitri wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed  Shein, akiteta jambo na  mwenyeji wake Kiongozi Mkuu katika Ofisi ya Rais Ikulu Nchini Vietnam,Bw Giang Son,wakiwa katika ukumbi wa Mapunziko  VIP  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali
Mama Mwanamwema Shein,(kulia) Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman,(atikati) na Balozi wa Tanzania Nchini China,pia akiwa anafanya kazi zake nchini Vietnam, Philip Sang'Ka Marmo,wakiwa katika Chumba cha Mapumziko  VIP  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam,wakiwa ni miongoni mwa Ujumbe wa Rais wa Zanzibar Nchini Vietnam
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Maofisa wa Serikali ya Vietnam, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekitri wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed  Shein,(katikati) akifuatana na mwenyeji wake Kiongozi Mkuu katika Ofisi ya Rais Ikulu Nchini Vietnam, Bw Giang Son,(wa pili kushoto) baada ya mapokezi rasmi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali,(kushoto) Balozi wa Tanzania Nchini China,pia akiwakilisha nchini Vietnam Philip Sang'ka Marmo.Picha Zote na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha:Majambazi Yafariki Kabla Ya Kufikishwa Hospitali


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha bunduki zilizokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambapo watatu kati yao walijeruhiwa kwa risasi na askari wa jeshi la Polisi na kisha kufariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali leo asubuhi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha kitako cha bunduki aina ya Rifle iliyokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. Watatu kati yao walijeruhiwa kwa risasi na askari wa jeshi la polisi na kisha kufariki dunia leo asubuhi
 Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ0 ambazo zilikutwa  kwenye begi la watu watano ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi .Tukio hilo lililtokea katika eneo la Olmatejoo jijini Arusha leo asubuhi na Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi Watatu kati yao ambao baadae walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.Picha na Mahmoud Ahmad-Arusha

Popular Posts